Dakshayani, anayefikiriwa kuwa tembo wa zamani kabisa duniani, amekufa akiwa na umri wa miaka 88 nchini India.

Kutokana na kichwa cha gaja Muthassi au kijana wa tembo, Dakshayani alishiriki katika ibada za hekalu na maandamano katika Hekalu la Chengalloor Mahadeva katika jimbo la kusini la Kerala.

Lakini mtunzaji na mwenye kumtibu tembo huyo alionekana naye mapema wiki hii akiwa amesimama naye huku akimpa chakula na inasemekana tembo huyo mzee alikufa Jumanne.

Wahifadhi wa tembo huyo walianza kumlisha mananasi na karoti miaka ya hivi karibuni baada ya kukabiliwa na tatizo la kushindwa huku na kule na kushindwa kuonekana hadharani na katika shughuli za kijamii kwa miaka kadhaa sasa.

Bodi ya Travancore Devaswom, ambayo inaendesha hekalu ambalo alikuwa akiishi tembo mzee, inaarifu kuwa tembo huyo ni wa zamani kabisa katika uhamisho na anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 88.Hata hivyo, mmiliki wa sasa wa Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa tembo wa zamani katika utumwa ni Lin Wang.

Tembo wa bara Asia alikufa kwenye bustani ya wanyama huko Taiwan mwaka 2003 akiwa mimwenye umri wa miaka 86, na kutumikia na wasifu wake uinaarifu kuwa kipindi cha uhai wake aliwahi kulitumikia Jeshi la Uingereza katika Vita Kuu vya Pili vya dunia.

Ndovu mwingine ni Indira, alikufa nchini India katika jimbo la Karnataka mnamo mwaka 2017 na iliripotiwa kuwa alikuwa mzee wa "kati ya miaka 85 ama 90".

KUSOMA ZAIDI  BOFYA BBC  Swahili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...