Polisi nchini Kenya wamewakamata watu saba wanaodaiwa kushirikiana kuigiza sauti ya rais Uhuru Kenyatta na maafisa wengine wa serikali katika kumuibia pesa nyingi mfanyabiashara tajiri nchini humo -Naushad Merali.
Mmoja wa watu hao alimpigia simu Bwana Merali, ambaye ni mwenyekiti wa Sameer Africa, akiigiiza sauti ya rais Uhuru kenyatta akimshawishi ampatie pesa za kusaidia mipango ya biashara, kulingana na polisi.
Fedha kamili zilizoibiwa bado hazijafahamika wazi - mtandao wa habari wa gazeti la Daily Nation news umeelezea kuwa zilikuwa ni shilingi milioni 10 ($100,000; £76,000) huku gazeti la Star likisema pesa hizo zilikuwa ni shilingi milioni 80.
Saba hao walifikishwa mhakamani Jumanne, lakini bado hawajashtakiwa.
Polisi wamesema wanahitaji musa zaidi wa kufanya uchunguzi.
"kutokana na ugumu wa uchunguzi na idadi ya washukiwa wanaohusika , wakiwemo wale ambao bado hawajapatikana , uchunguzi unatarajiwa kujumuisha nyaraka nyingi zikiwemo zile za benki pamoja na uchunguzi wa kina wa data za mawasiliano simu ," ilieleza ripoti ya polisi iliyonukuliwa na gazeti la Daily Nation.
KUSOMA ZAIDI BOFYA BBC Swahili.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...