Jumla ya wanafunzi 52
wa stashahada ya ualimu kutoka katika chuo cha ualimu cha Monduli
wamefika katika ofisi za Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, Makao
Makuu Njiro Arusha kwa lengo la
kujifunza kwa vitendo masuala mbali mbali ya kisayansi ambayo wamekuwa
wakiyasoma katika nadharia.
Lengo la ziara hii ya siku
moja kwa wanafunzi hawa ni kujifunza ili kufahamu dhana nzima ya juu ya
matumizi salama ya mionzi na namna udhibiti unavyofanyika na wao kuwa mabalozi wazuri
katika uhamasishaji wa matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia.
Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Profesa Lazaro Busagala amewaeleza
wanafunzi hao kuwa elimu waliyoipata katika ziara hii ya mafunzo itawawezesha kuelewa
matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia na kujilinda na mionzi pindi
watakapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kikazi hapo
baadaye.
Kiongozi wa
wanafunzi hao Mwalimu Sikana Menard
ameeleza kuwa ziara hiyo imewasaidia wanafunzi hao ambao ni walimu watarajiwa
hapo baadae katika masomo ya sayansi kuwa wamepata elimu kubwa kuhusiana na masuala ya mionzi.
Amesema
wamekuwa wakiwafundisha wananfunzi kwa njia ya nadharia tu hivyo kwa kutembelea
kwenye Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania kutawasaidia sana kujionea teknolojia
mbali mbali katika maabara za TAEC zenye ubora wa hali ya juu kwa ajili ya
mafunzo.
Aidha TAEC
inaendelea kuwakaribisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali ili kujipatia
elimu na kujifunza masuala tofauti tofauti yanayohusu udhibiti salama wa mionzi
na matumizi salama ya teknolojia ya
nyuklia hapa nchini.
Imetolewa
na;
Peter G. Ngamilo
Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano
Tume ya Nguvu za Atomiki
Tanzania.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...