Wataalam wa Radiolojia wakijengewa uwezo wa namna ya kutoa sampuli kwa kuongozwa na mashine ya Utrasound.
Waalam wa Radilojia kutoka Marekani pamoja na wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila wakisoma kipimo cha Mamografia ili kubaini uvimbe uliopo kwenye matiti.
Dkt. Mwajuma Jumbe akitumia mashine ya Utrasound kupima uvimbe kwenye titi ili kubaini sehemu ambayo uvimbe upo.
Dkt. Tim Rooney (kulia) pamoja na Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila wakitoa sampuli ya uvimbe kwenye titi bila kufanya upasuaji (Core Biopsy) kwa kuongozwa na mashine ya Utrasound leo hospitalini hapo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru akipokea maelezo mara baada ya kuwasili kwa timu ya watalaam wa Radiolojia kutoka nchini Marekani.
Timu ya watalaam wa Radiolojia kutoka nchini Marekani wamewasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila kwa ajili ya kuwajengea uwezo watalaam wa hospitali hiyo wa kutoa sampuli kwenye vivimbe vya kwenye matiti kupitia njia ya kitaalam (Core Biopsy).
Watalaam hao kwa kushirikiana na wataalam wa Hospitali ya Mloganzila watatoa sampuli kwa watu zaidi ya 50 ambao wana vivimbe kwenye matiti ambapo watashirikiana kutoa huduma hiyo kwa zaidi ya wiki mbili.
Februari 02 hadi Februari 03 mwaka huu Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila kwa kushirikiana na Madaktari kutoka Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania-MEWATA- walitoa huduma bure ya uchunguzi awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti.Katika zoezi hilo watu zaidi ya 130 walifanyiwa uchunguzi, kati ya hao 36 wamekutwa na vivimbe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...