Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akisikiliza mapendekezo mbalimbali yaliyokuwa yanawasilishwa na watumishi wa Tume ya Madini (hawapo pichani).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akifafanua jambo katika kikao hicho.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya akiwatambulisha viongozi wa Tume ya Madini pamoja na wafanyakazi.
Kutoka kushoto, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Waziri wa Madini, Doto Biteko na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na wafanyakazi wa Tume.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akizugumza na watumishi wa Tume ya Madini (hawapo pichani).
Watumishi wa Tume ya Madini wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani)
Watumishi wa Tume ya Madini wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani)
Waziri wa Madini, Doto Biteko leo tarehe 06 Februari, 2019 amekutana na watendaji na watumishi wa Tume ya Madini katika makao makuu ya Tume yaliyopo jijini Dodoma, lengo likiwa ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Tume.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Madini, Issa Nchasi na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula.
Wengine ni pamoja na Kamishna kutoka Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya, Wakurugenzi, Mameneja pamoja na watumishi wa Tume ya Madini.
Katika kikao hicho Waziri Biteko ametoa maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vituo vya ukaguzi wa madini ya ujenzi kufufuliwa, kikao cha kamati tendaji kukutana mara kwa mara kwa ajili ya kupitia na kuidhinisha maombi mbalimbali ya leseni za madini na watumishi kufanya kazi kwa uadilifu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...