Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
leo amewaongoza watumishi wa wizara hiyo katika hafla fupi ya kumuaga rasmi aliyekuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Mpoki Ulisubisya ambae ameteuliwa kuwa
Balozi.
Wakati huo huo aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Wizara ya Afya, ambaye
amekuwa Naibu Katibu Mkuu Idara ya Afya TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima na
kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na aliyekuwa Naibu Katibu
Mkuu Idara ya Afya TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula ambaye kwa sasa ni Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara
Kuu ya Afya na aliyekuwa Mganga Mkuu wa Dar es salaam ambaye kwa sasa ni
Kaimu Mkurugenzi wa Idara Tiba Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe
Katika hafla hiyo Waziri Ummy amewashukuru watumishi wote wakiongozwa na Dkt Mpoki Ulisubisya kwa ushirikiano waliouonesha katika kipindi chote walichofanya kazi Wizara ya Afya na kuwasihi kuendeleza uchapaji kazi ili kusukuma gurudumu la Maendeleo hususani maendeleo ya Sekta ya Afya.
Aidha, Waziri Ummy amewakaribisha Watumishi wote walioamia katika Wizara ya Afya, Waziri Ummy amesema kwamba licha ya mafanikio makubwa ambayo Sekta ya Afya imepiga, bado kuna changamoto nyingi ambazo zinapaswa kutatuliwa ikiwemo suala la uhaba wa watumishi, na upatikanaji wa Dawa na vifaa tiba.
Naye Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Fustine Ndugulile amewakumbusha Watumishi wa Sekta ya Afya juu ya uwajibikaji na kuwatoa hofu kuwa, kama Serikali milango yao ipo wazi muda wote, hivyo kwa yoyote mwenye wazo zuri la kujenga na kuipeleka mbele Sekta ya Afya asisite kuwaona.
Kwa upande wake, aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya amewashukuru Watumishi wote wa Sekta ya Afya wakiongozwa na Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu kwa ushirikiano waliomuonesha katika kipindi chote alichohudumu katika Wizara ya Afya, kisha kuahidi kuwa Balozi Mzuri huko atakoenda ili kuikuza Sekta ya Afya.
Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula amewakumbusha Watumishi wa Sekta ya Afya juu ya umoja na ushirikiano baina yao, huku akisisitiza kila mmoja ni lazima ahakikishe anatimiza wajibu wake ili kusukuma mbele Maendeleo ya Sekta ya Afya.
Kwa upande wake, aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Wizara ya Afya ambae sasa ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Idara ya Afya Dkt Dorothy Gwajima ameahidi kuwa daraja zuri na imara baina ya Wizara ya Afya na TAMISEMI kutokana na kuzijua Wizara zote mbili kiundani na kuahidi kuendeleza mazuri yote yalioachwa na Dkt. Zainab Chaula.

wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mhe.Ummy Mwalimu
akimkabidhi Zawadi Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa Hafla ndogo ya
kumuaga yeye na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla
ya kuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya
wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu
akisaini Biblia Takatifu aliyopewa kama zawadi Balozi Dkt. Mpoki
Ulisubisya wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Baozi Dkt Mpoki Ulisubisya
Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika
nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula, hafla ilofanyika katika ofisi za
Wizara ya Afya jijini Dodoma.

Wakwanza
kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mhe.Ummy Mwalimu akifuatilia alichakuwa akiongea Mganga Mkuu wa Serikali
Prof. Muhammad Bakari Kambi wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Balozi Dkt
Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya
kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi
wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula
(Wakatikati) na (Wakwanza kishoto) ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Idara
ya Afya Dkt Dorothy Gwajima.

Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu
(kushoto) akiwa na Naibu wake Dkt. Faustine Ndugulile (kulia)
wakifuatilia alichakuwa akiongea Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad
Bakar Kambi (hayupo pichani) wakati wa hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki
Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla
yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya
wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula.

Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akisisitiza jambo wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga
Balozi Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara
ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha
Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab
Chaula.

Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu
akisisitiza jambo wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Balozi Dkt Mpoki
Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla
yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya
wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula.

Mkurugenzi
wa MSD ambae pia ni mwakilishi wa Wakurugenzi wa Taasisi zote za Wizara
ya Afya Laurean Bwanakunu akitoa salamu za taasisi zote za Afya wakati
wa Hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima
waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na
kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Dkt Zainab Chaula, hafla hiyo imefanyika katika ofisi za Wizara ya Afya
jijini Dodoma.

Baadhi
ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Waziri Ummy wakati wa Hafla
ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima
waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na
kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Dkt Zainab Chaula. Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Wizara ya Afya

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Idara ya Afya Dkt Dorothy Gwajima.

Aliyekuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya akiteta jambo
na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi wakati wa Hafla
ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima
waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na
kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Dkt Zainab Chaula, hafla ilofanyika katika ofisi za Wizara ya Afya
jijini Dodoma.

Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu
akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula wakati wa
Hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima
waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na
kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Dkt Zainab Chaula.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...