Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa
pole JR Hamisi Kigwangalla kufuatia kifo cha mdogo wake Zul, kulia ni
Baba wa Marehemu Zul, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt Hamisi
Kigwangalla muda mfupi kabla ya mazishi yaliofanyika Puge wilayani Nzega
mkoa wa Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akimpa mkono wa pole Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt
Hamisi Kigwangalla kufuatia kifo cha mtoto wake mdogo wa kiume Zul muda
mfupi kabla ya mazishi Puge wilayani Nzega mkoa wa Tabora.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza
Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Bashe mara baada ya kuweka
jiwe la msingi la uzinduzi wa kiwanda cha kuchakata gesi, kushoto ni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri (kulia)Makamu
wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za
kimaendeleo mkoani Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na
Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara, Mbunge wa Igalula Mhe. Mussa
Ntimizi (kulia) na Mkuu Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri, Mkuu wa
Wilaya ya Uyui Bi. Gift Msuya (kushoto) mara baada ya ukaguzi wa
maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Igalula, wilayani Uyui mkoa wa
Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...