Katibu
Mkuu wizara ya maliasili na utalii Prof.Adolf Mkenda amesema kuwa
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Grumeti Fund inatarajia kuingiza faru 10
nchini kwa ajili kuongeza idadi ya wanyama hao hapa nchini.
Kuagizwa kwa Faru hao kutaongeza idadi yao kutoka 2 walioagizwa na taasisi hiyo hapo awali hadi kufikia 12.
Akizungumza katika kikao kilichowahusisha wadau hao wa uhifadhi kilichofanyika katika chuo cha Uhifadhi wa Wanyamapori cha Pasiansi jijiji mwanza, Prof. Mkenda amewashukuru wadau hao kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha shughuli za uhifadhi nchini.
Amesema Serikali itaendeleza mahusiano mazuri yaliyopo baina yake na wadau wote wapenda maendeleo kwa lengo la kulinda na kukuza shughuli za uhifadhi wa wanyamapori nchini.
Prof. Mkenda amesema kuwa kuletwa kwa faru hao kutaongeza idadi ya wanyama hao hapa nchini na kuongeza kuwa taasisi ya Grumeti imesaidia kuwaleta watu maarufu kutoka katika mataifa mbalimbali kuja kutembelea hifadhi za Taifa na hivyo kuchangia kutangaza utalii na kuongeza pato la Taifa.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa idara ya wanyamapori Tanzania Canisius Karamaga akizungumzia kuhusu ujio wa Faru hao amesema kuwa jitihada zinazofanywa na taasisi hiyo zinalenga kuwaongeza Faru hao hapa nchini.
Ameongeza kuwa Faru hao wataingizwa nchini kwa lengo la kuboresha kizazi cha wanyama hao waliokuwa hatarini kutoweka ikiwa ni moja ya juhudi za kuwafanya waongezeke kwa kuzaliana na wale waliopo nchini.
Amesema kikao hicho kati ya wizara na wadau hao ni muhimu sana kwa kuwa kimejadili na kuangalia kwa utalaam Zaidi namna Faru hao watakavyoingizwa nchini, kutunzwa na kulindwa kwa kuwa wanyama hao ni adimu na muhimu kwa utalii.
Amewataka watanzania kuwa mstari wa mbele kulinda rasilimali za nchi ili ziwe na faida kwa vizazi vijavyo.

Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda akisalimiana na
watumishi wa Wizara hiyo kutoka katika taasisi za Uhifadhi wa
Wanyamapori na wadau kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya Grumeti Fund
inayotarajia kuingiza faru 10 kwa ajili kuongeza idadi ya wanyama hao
hapa nchini.
Wadau
wa Uhifadhi kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya Grumeti Fund
wakifuatilia kikao cha pamoja kilichowahusisha viongozi wa Wizara ya
Maliasili na Utalii na watumishi wa Wizara hiyo kutoka katika taasisi za
Uhifadhi wa Wanyamapori, kikao hicho kimefanyika katika Taasisi ya
Taaluma ya Wanyamapori, Pasiansi jijini Mwanza.
Baaadhi
ya Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoka katika taasisi za
Uhifadhi wa Wanyamapori wakiwa katika kikao cha pamoja na Wadau wa
Uhifadhi kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya Grumeti Fund
kilichofanyika katika Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori, Pasiansi jijini
Mwanza.PICHA/ Maliasili na Utalii-Mwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...