Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka katika kesi ya kutumia lugha chafu ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kuhakikisha tarehe ijayo kesi hiyo inasikilizwa.

Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba ameyasema hayo leo Machi 21, mwaka huu kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa na wakili wa serikali Dasy Makakala ambayo ameiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo kwa kuwa faili hilo lilikuwa kwa wakili mwingine na bado hajalipitia.
Wakili wa utetezi, Hekima Mwesipu alidai, shauri hilo ni la muda mrefu kwani limebakiza miezi minne tu kufikisha miaka miwili huku ikiwa haijamaliza kusikilizwa hivyo ameomba hili liwe ahirisho la mwisho.

Baada ya kusema hayo, Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 16, 2019.

Katika kesi hiyo tayari mashahidi watatu wa upande wa mashtaka wamekwishatoa ushahidi akiwamo  mkuu wa Kituo cha Polisi cha Urafiki, Mrakibu wa Polisi (SP) Batseba Kasanga.

Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa Julai 3, 2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni, Mdee anadaiwa kutamka maneno dhidi ya  Rais John Magufuli kuwa  “anaongea hovyohovyo , anatakiwa  afungwe breki”  na kwamba kitendo ambacho kingeweza  kusababisha uvunjifu wa amani.  

Mdee alifikishwa mahakamani hapo Julai 10, 2017 na yupo nje kwa dhamana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...