Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(kushoto) akiongoza Kikao cha 40 cha kujadili Wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole. Kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Kamishna wa Magereza, Uwesu Ngarama ambaye pia ni Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole. Kikao hicho cha siku moja kimefanyika leo Machi 8, 2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza, Kamishna wa Magereza, Uwesu Ngarama ambaye pia ni Kaimu Katibu
wa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole akitoa taarifa fupi ya
Sekretarieti kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya
Parole, Mhe. Augustino Mrema(hayupo pichani)afungue rasmi kikao hicho.
Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya
Parole wakifuatilia majadiliano ya wafungwa waliopendekezwa
kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole leo Machi 8, 2019, katika
Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Ujumbe kutoka Zanzibar
wakishiriki mazungumzo maalum yenye lengo la kubadilishana uzoefu na
Bodi ya Taifa ya Parole Tanzania katika ziara yao ya kikazi leo Machi 8,
2019. Wa kwanza kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Said
Hassan(katikati) ni Waziri wa TAMISEMI na Vikosi Maalum vya Zanzibar,
Mhe. Haji Omari na Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Polisi kutoka Zanzibar,
Hasina Ramadhani.
Sekretarieti wakifuatilia kwa makini majadiliano katika kikao hicho.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya
Parole, Mhe. Augustino Mrema(wa nne toka kushoto walioketi) akiwa katika
picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole pamoja na
Viongozi Waandamizi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, leo Machi 8,
2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga, Jijini Dar es
Salaam baada ya ufunguzi wa Kikao cha Bodi ya Taifa ya Parole(Picha zote
na Jeshi la Magereza).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...