Kocha Mkuu wa Taifa Stars Emmanuel
Amunike akiwa na Rais wa TFF Wallace Karia
Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti inakabiliwa na mchezo muhimu dhidi ya Uganda wa kufuzu kucheza Fainali za Afrika mwaka huu. Huu ni mchezo ambao kama Taifa Stars itashinda inaweza kukata tiketi ya kucheza AFCON mwaka huu itakayofanyika nchini Misri. 
 Mchezo dhidi ya Uganda utachezwa Jumapili Machi 24,2019 saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Taifa na leo  Kocha Mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike ametangaza kikosi kitakachopambana kuisaka tiketi hiyo kwenye Uwanja wa nyumbani. 
 Nahodha Mbwana Samatta anayecheza KRC Genk ya Belgium ataongoza kikosi katika mchezo huo uliobeba imani ya Watanzania.

Kocha Amunike amesema Kikosi alichokitaja kimezingatia mambo mengi kuhakikisha Taifa Stars inapata ushindi. Amewataka Watanzania kuiunga mkono Taifa Stars katika kuipeperusha bendera ya Tanzania. 

 Kwa upande wake, Afisa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), George Mango amesema kampuni hiyo imekuwa ikihakikisha kikosi hicho kinafanya maandalizi mazuri ili kufanya vema kwenye mchezo ujao na hatimaye iweze kuibuka na ushindi na kukata tiketi kucheza Afcon. 

 “Siku zote kinywaji cha Serengeti Premium Lager ni shabiki mkuu wa Taifa Stars na mdhamini mkuu pia. Katika mchezo huu tumejidhatiti kuhakikisha timu yetu inaibuka na ushindi ambao utakuwa fahari kwa Taifa letu na kwa kinywaji chetu cha Serengeti,” alisema Mango. 

 Mango aliwataka mashabiki wa soka nchini kufika kwa wingi siku ya mchezo huo ili kuwapa hamasa wachezaji kwaajili ya kuipa ushindi timu hiyo ya Taifa.

Kikosi cha Taifa Stars kilichoitwa:
1.Aishi Manula -Simba 
2.Feisal Salum -Young Africans 
3.Hassan Kessy-Nkana,Zambia 
4.Yahya Zayd-Ismaily,Misri 
5.Gadiel Michael-Young Africans 
6.Himid Mao-Petrojet,Misri 
7.Mudathir Yahya-Azam FC 
8.Shaaban Chilunda-Tenerife,Hispania 
9.Kelvin Yondan-Young Africans 
10.Shiza Ramadhan-ENPPI,Misri 
11.Simon Msuva-El Jadida,Morocco 
12.Rashid Mandawa-BDF,Botswana 
13.Jonas Mkude-Simba 
14.Mbwana Samatta-KRC Genk,Belgium 
15.Thomas Ulimwengu-JS Saoura,Algeria 
16.Mechata Mnata-Mbao FC 
17.Aron Kalambo-Tz Prisons 
18.Suleiman Salula-Malindi FC,Zanzibar 
19.Vicent Phillipo-Mbao 
20.Ally Mtoni-Lipuli 
21.Andrew Vicent-Young Africans 
22.Kennedy Wilson-Singida United 
23.Aggrey Morris-Azam FC 
24.John Bocco-Simba 
25.Farid Mussa-Tenerife,Hispania 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...