Sehemu ya washiriki wa warsha ya siku moja iliyolenga kutathimini mustakabali wa juhudi za ukombozi wa mwanamke nchini kuelekea miaka 25 ya mkutano wa Beijing hapo mwakani.
Mwenyekiti
wa TGNP Mama Assen Muro akitoa rai kwa wadau wote kuhakikisha
wanatafuta ufumbuzi wa changamoto zinazosimama kama vikwazo ili wanawake
waweze kupiga hatua katika kufikia maendeleo endelevu.
Mwenyekiti wa TGNP Mama Assen Muro akimueleza jambo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa alipowasili kwenye warsha hiyo.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu,
Mhe. Stella Ikupa akizungumza na washiriki wa warsha hiyo ambapo
aliwahimiza kutorudi nyuma katika jitihada za kutetea haki na nafasi ya
mwanamke katika jamii.
Na Mwandishi Wetu,
Ikiwa
ni wiki ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kilele ni
tarehe 8 ya mwezi Machi kila mwaka,wadau mbali mbali wamekutana jijini
Dodoma kujadili na kutathimini mustakabali wa juhudi za ukombozi wa
mwanamke nchini kuelekea miaka 25 ya mkutano wa Beijing hapo mwakani.
Warsha hiyo siku moja ambao iliyowakutanisha washiriki zaidi ya 100 kutoka kote nchini wakiwemo wadau
mbalimbali likiwajumuisha wanawake wakiwakilisha makundi mbalimbali,wabunge,madiwani,wanasheria,waandishi wa habari pamoja na
wanafunzi wa vyuo na sekondari,iliandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na TAWLA, Landesa, Msichana Initiative, Haki Ardhi, Haki Elimu, Care International na TAMWA.
Mkutano
huo wa Beijing uliofanyika mwaka 1995 ulilenga kuwashirikisha na
kuwawezesha wanawake katika maendeleo ili kuimarisha mapambano dhidi ya
umaskini na hiyo yote ni kwa wanawake kushiriki katika shughuli za
kimaendeleo.
Katika
kuhakikisha kila mshiriki anachangia mawazo,ilitumika njia ya kuwagawa
katika makundi na kujadili maana,uelewa,umuhimu,mitizamo pamoja na
changamoto la azimio la Beijing katika jamii na nchi kiujumla ambapo
miongoni mwa hoja zilizoibuliwa katika kuboresha jitihada za kuleta
usawa wa kijinsia ni pamoja na elimu juu ya azimio bado inahitajika
sambamba na ushirikishwaji wa jamii yote kwa ujumla sambamba na kueleza
faida ya usawa wa kijinsia kuanzia ngazi ya familia ili kutengeneza
kizazi chenye kuelewa manufaa yake.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanasimamiwa na kauli mbiu inayosema “Badili fikra kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu”.
Mkutano huo wa Beijing uliofanyika mwaka 1995 ulilenga kuwashirikisha na kuwawezesha wanawake katika maendeleo ili kuimarisha mapambano dhidi ya umaskini na hiyo yote ni kwa wanawake kushiriki katika shughuli za kimaendeleo.
Wawakilishi wa wanawake wa jamii ya wafugaji wilayani Mvomero wakiongozwa na mwenyekiti wa umoja huo Bi. Mariam Simango (wakwanza kushoto) wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika warsha hiyo.
Akifafanua
lengo la warsha hiyo, Mary Ndaro kutoka Care International aliwaambia
washiriki kwamba warsha hii ni fursa kwa wanawake kurejea azimio la
Beijing imefanikiwa kwa kiasi gani na kujua ni zipi jitihada za kuongeza
ili kuendelea kuikwamua hali ya mwanawake katika jamii .
Kundi
liliojumuisha wanafunzi katika ngazi zote pamoja na vijana likiwa
makini kujadili mitazamo na uelewa juu ya azimio la Beijing ambapo
kufikia 2020 litatimiza miaka 25 ya maazimio.
Akichangia
wakati wa majadiliano ya katika makundi,mbunge wa Mtera Mhe.Livingstone
Lusinde alisisitiza kuwa azimio la Beijing halina azma ya kuwafukuza
wanaume kutoka nafasi zao katika jamii, bali ni juu ya kuinua wanawake
kwa hali ya juu ili waweze kupata haki zao kama wanaume na kufanya kazi
pamoja kwa maendeleo ya nchi.
Anna
Marwa kutoka Pelum Tanzania akichangia jambo wakati wa majadiliano ya
makundi yaliyolenga kupima umuhimu,mitazamo na uelewa juu ya azimio la
Beijing miongoni mwa washiriki wa warsha hiyo.
Zawadi
Kondo mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha
majibu kwa niaba ya kundi lililojumuisha wanafunzi katika ngazi zote
pamoja na vijana.
Washiriki wakifuatilia kwa karibu mawasilisho.
Mdau
wa masuala ya wanawake ambaye pia ni mwandishi wa habari wa gazeti la
Mwananchi Rachel Chibwete akiwasilisha majibu kwa niaba ya kundi
lililojumuisha wabunge,madiwani pamoja na waandishi wa habari.
Wanafunzi
kutoka shule ya sekondari Manchali iliyopo Chamwino jijini Dodoma
wakicheza kuashiria furaha yao kutokana na fursa ya kushiriki katika
warsha hiyo.
Washiriki
wakishikana mikono kama ishara ya umoja na mshikamano ambayo kwa pamoja
waliafiki kuwa ni nguzo muhimu katika kufanikiwa kuitetea nafasi ya
mwanamke katika jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...