Baadhi ya wakinamama kutoka kijiji cha kijiji cha Engikaretia wilayani Longido wanavyoonekana wakiteka maji
Na. Vero Ignatus, Longido
Kamati
ya kudumu ya Bunge ya Uvuvi na mifugo na Maji imetembelea na kukagua
mradi ya maji mji mdogo wa Longido ili kuona umefikia hatua gani
kimaendeleo
Akisoma
ripoti ya maendeleo ya mradi huo Mkurugenzi wa AUWSA Jijini Arusha
Mhandisi Ruth Koya amesema kuwa serikali kupitia wizara ya maji na
umwagiliaji inatekeleza mradi wa maji safi na salama katika mji mdogo wa
Longido ambapo chanzo chake ni mto Simba uliopo Wilaya ya Siha mkoani
Kilimanjaro
Amesema
mradi huo unategemewa kugarimu kiasi cha shilingi Bilioni 15.8 ambapo
hadi sasa kiasi cha shilingi bilioni 12.3 kimeshalipwa kwa mkandarasi.
Mhandisi
Koya amesema kuwa lengo kuu la mradi ni kuongeza upatikanaji wa maji
katika mji mdogo wa Longido kutoka 15%za sasa ambazo ni sawa na wakazi
2, 510 hadi kufikia 100%sawa na wakazi. 16 712 ambapo kiasi hicho
kitatosheleza kwa 100% hadi kufikia wakazi 26,145 mwaka 2025
Ameiambia
kamati hiyo ya Bunge kuwa mradi huo unauwezo wa kuzalisha kiasi cha
lita za ujazo 2,160 kwa siku na mahitaji ya maji ni lita za ujazo 1462
hivyo itaongeza upatikanaji wa huduma ya maji katika mji mdogo wa
Longido wenye jumla ya wakazi 16, 712 kwa sasa, na kufikia wakazi 26,
145 kwa mwaka 2025
Aidha
amesema kuwa mradi huo utaondoa magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa
maji safi na salama kwa kijiji cha Engikaretia mbapo utahudumia wakazi
wapatao 1294
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kamati uya kudumu ya bunge ya Uvuvi, Mifugo na Maji Mahmoud Mgimwa amesema kuwa mradi huo unapokamilika siyo wa serikali bali wenye jukumu la kuutunza na kuulinda ni wananchi wa Longido.
Amewahakikishia
wananchi hao kuwa tayari kamati hiyo imeshazungumza na serikali kuwa
ifikapo machi 30 mwaka huu mradi huo utakuwa umeshakamilika na kwamba
watarudi tena kwenda kuhakikisha kama kuna mgao wa maji katika maeneo
yao.
''
Leo tumekuja kukagua na kuona tumefikia kwa asilimia ngapi, na mkiona
kuna uharibifu wa aina yeyote na nyie mkaa kimya na nyie mtakuwa sehemu
ya uharibifu''alisema Katibu huyo
Aidha
Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge imemuagiza DC wa Longido pale atakapoona
uharibifu wowote kwenye eneo la mradi kuwachukulia hatua za kisheria
watu wote waliopo eneo hilo.
Akizungumza
bi Lucy Martini mkazi wa Longido ameiomba kamati hiyo kuhakikisha mradi
huo uwe unatoa maji mara zote isijeikawa ni kwa siku moja tu halafu
hapo baadae tatizo la. Maji likarudi palepale.
Mkurugenzi
wa AUWSA jijini Arusha akitoa taarifa ya mradi wa maji mji mdogo wa
Longido kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uvuvi, Mifugo na Maji leo
wilayani Longido.
Mkurugenzi wa AUWSA jijini Arusha Mhandisi Ruth Koya akiwa na Katibu wa Kamati ya Bunge ya Uvuvi, Mifugo na Maji
Mradi wa maji katika kijiji
cha Engikaretia kilichopo mji mdogo wa Longido utakaogharimu kiasi cha
shilingi Bilioni 15.8 ambapo hadi sasa tayari makandarasi ameshalipwa
shilingi bilioni 12.3
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Uvivu, Mifugo na maji akizungumza na
wananchi mji mdogo wa Longido leo,kushoto kwake ni Kaimu katibu mkuu
wizara ya maji Emmanuel Kalobelo naibu katibu Mkuu Wizara ya maji mradi
Emmanuel Kalobelo. Picha na Vero Ignatus.
Mkuu wa wilaya ya Longido akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akinamama waliokuja kuteka maji katika kijiji cha Engikaretia mji mdogo wa Longido leo Picha zote na Vero Ignatus
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...