Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii  

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Mwekezaji wa Klabu ya Soka ya Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ kwa mara ya kwanza ameonyesha hisia zake na mapenzi kwa klabu hiyo katika mchezo wa mwisho wa Kundi D la Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club ya DR Congo, ambapo Simba SC iliondoka na ushindi wa bao 2-1 na kufuzu Robo Fainali ya Michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya klabu.
Katika mchezo huo uliopigwa dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam majira ya Saa 1 Usiku, Simba SC ilionyesha kiwango bora na kupata ushindi huo mbele ya timu ngumu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Vita Club.

Mohammed Dewji ‘MO’ akiwa na furaha iliyoje! siku hiyo baada ya ushindi huo wa Simba SC, MO ametuma picha yenye ujumbe iliyojawa na hisia ya huzuni na masikitiko kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Instagram wakati huo kabla pambano kumalizika.

Ujumbe huo umeandikwa hivi: ‘’Hizi Picha zilipigwa zikiwa zimebaki dakika 3 kabla ya mpira kuisha. Tulikuwa na wasiwasi, Pressure ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba vidole vilikuwa na ganzi. Somo: Usikate tama. Mipango ya Mungu haina makosa! AMEEN’’

Baada ya matokeo hayo, Simba SC imetinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano hiyo, hata hivyo itasubiri March 20  droo ya Robo Fainali itakayofanyika nchini Misri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...