Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Rais Mstafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete(MB) Wameongoza Maelfu ya Watanzania katika kuaga Mwili wa aliyekuwa Mtangazaji wa kituo cha Clouds Fm Marehemu Ephraim Kibonde nyumbani kwa Baba yake Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam.
Katika ibada hiyo ya kutoa aheshima za mwisho viongozi wengine wa kiserikali waliohudhuria ni pamoja na Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo , Dr Harrison Mwakyemb, Waziri wa Madini Doto Biteko,Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ,Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda , Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo.
Viongozi wengine waliofika katika Msiba huo ni pamoja na Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Suleiman Jaffo, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.
Aidha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini kwa umoja wao walifika katika msiba huo na kutoa faraja kwa wafiwa ambapo safari ya kuelekea Makaburi ya kinondoni kumpumzisha mpendwa wetu Ephrahim Kibonde.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Samson Job Kibonde(kushoto) ambaye ni baba mzazi wa aliyekuwa Mtangazaji wa Clouds FM, Marehemu Ephraim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani kwao marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia, Machi 9, 2019. Kulia ni Mkurugenzi wa Clouds Media, Joseph Kusaga
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha
Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani kwao
marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia,
leo Machi 9, 2019.
Mke
wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete(MB) akisaini kitabu cha Maombolezo
wa Ephrahim Kibonde nyumbani kwa Baba yake Mbezi Beacha Jijini Dar es
Salaam.
Rais
Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili nyumbani kwa alieyekuwa
mtangazaji wa Clouds FM, Merehemu Ephraim Kibonde leo Mbezi Beach jijini
Dar es salaam kutoa pole kwa familia, Machi 9, 2019. Wa kwanza kulia ni
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe
na kushoto ni Mkurugenzi wa Clouds Media,
Joseph Kusaga
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitoa pole kwa Mkurugenzi wa Clouds Media,
Joseph Kusaga alipowasili nyumbani kwa alieyekuwa
mtangazaji wa Clouds FM, Merehemu Ephraim Kibonde leo Mbezi Beach jijini
Dar es salaam kutoa pole kwa familia, Machi 9, 2019. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Samson Job Kibonde(kushoto) ambaye ni baba mzazi wa aliyekuwa Mtangazaji wa Clouds FM, Marehemu Ephraim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani kwao marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia, Machi 9, 2019. Kulia ni Mkurugenzi wa Clouds Media, Joseph Kusaga
Rais
Mstafu wa Awamu ya tatu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma
Kikwete(MB), Wakizungumza na Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph
Kusaga mara baada ya kusaini kitabu cha Maombolezo.
Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara akitoa pole kwa Dada wa Marehemu Sara Kibonde wakati wa zoezi la kuaga mwili wa Marehemu Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiteta jmabo na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makzi mara baada yakuaga Mwili wa Marehemu Ephrahim Kibonde.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondomni Daniel Chongolo akibadilishana mawazo na Wadau wa habari waliofika katika Msiba wa Ephrahim Kibonde
Mmoja wa Waombolezaji wakifika Msibani huku wakiwa wanasaidiwa na wanandugu wengine
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...