UTANGULIZI
Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki inatangaza mafunzo katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini
Israel. Mafunzo hayo ni ya miezi 11 kuanzia mwezi Septemba, 2019 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Serikali ya Israel kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mafunzo hayo yatahusisha pia vitendo (field attachment) kwenye mashamba
makubwa ya mazao mbali mbali yakiwemo ya matunda, mbogamboga, ufugaji, uvuvi na
mazao mengine ya biashara kwa ujira maalum.
SIFA NA VIGEZO VYA MWOMBAJI
ii.
Awe amehitimu mafunzo ya
Kilimo katika ngazi ya shahada ya Chuo Kikuu, Stashahada au Astashahada ya Vyuo
vya kilimo vinavyotambulika nchini.
iii.
Awe na afya njema.
iv.
Awe na ujuzi wa kuandika
na kuongea lugha ya Kiingereza.
v.
Awe na uwezo wa kufanya kazi
na watu wa tamaduni mbalimbali.
vi.
Awe tayari kurejea nchini
baada ya mafunzo yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...