Na Jumbe Ismailly SINGIDA
MAMLAKA
ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Kati Dodoma imeanza kutoa mafunzo ya
namna ya kudhibiti natumizi ya vyakula,dawa,vipodozi pamoja na
vitendanishi kwa lengo la kutoa elimu kwa shule 30 za sekondari zenye
jumla ya wanafunzi 12,000.
Mkaguzi
wa TFDA Kanda ya Kati,Abeli Daule aliyasema hayo alipokuwa akitoa elimu
juu ya bidhaa ambazo Mamlaka ya Chakula naa Dawa inadhibiti zikiwemo
bidhaa za chakula,dawa,vifaa tiba na vitenganishi katika shule nane za
sekondari za Halmashauri ya wilaya ya Singida.
Aidha
Daule ambaye pia ni Afisa elimu kwa umma wa TFDA aliweka bayana lengo
la kutoe elimu katika shule za sekondari kuwa ni sehemu za kazi ya
Mamlaka hiyo kutoa elimu na kwamba sekondari ni wanafunzi wengi ambao
tayari wanajitambua, kukiwepo watumiaji.
“Lakini
pia sekondari wanafunzi ambao wengi tayari wanajitambua kwa maana
kwamba wengine ni watumiaji lakini na wengine majumbani kwao
wanatumwa,lakini pia ni muda ambao wakipewa elimu wanaweza kujua kufanya
uchaguzi sahihi lakini pia watapeleka elimu hiyo nyumbani.”alisisitiza
Mkaguzoi huyo.
Kwa
mujibu wa Daule endapo wanafunzi hao wa sekondari watapatiwa elimu
itasaidia pia kwa namna moja au nyingine kuwadhibiti wafanyabiashara
wasio waaminifu wenye utamaduni wa kuikwepa serikali wanapobaini Mamlaka
hiyo inafanyakazi, huamua kufunga biashara zao kutoweka kabisa.
“Kwa
hiyo utaratibu huo ni wa taasisi kwa maana kwamba Mamlaka ya Chakula na
Dawa (TFDA) Kanda ya Kati katika utekelezaji wa robo ya nne ya mwaka wa
fedha 2018/2019 basi tumeona tupite katika hizi shule ili tuweze
kuwapitia.”alibainisha Daule.
Naye
Kaimu Afisa elimu sekondari wilaya ya Singida,Wolta Jenaeli aliweka
bayana manufaa ya mpango huo utasaidia kwa akiasi kikubwa sana kwenye
shule 30 zilizopo katika Halmashauri hiyo kupunguza madhara yatokanayo
na vipodozi hususani kwa wanafunzi wa kike ni makubwa sana.
“Kwa
hiyo ina maana tunapunguza zinazotokea kwenye mashule yetu kwa sababu
umri wa watoto wetu walionao kutumia kila kitu bila kujua madhara yake
ni yapi.”alisema kaimu afisa elimu wilaya ambaye pia ni afisa elimu
sekondari wa wilaya hiyo.
Alizitaja
baadhi ya shule za sekondari zilizopatiwa elimu hiyo kutoka TFDA kuwa
ni pamoja na Ntonge,Amana,Mrama,Kijota, Kijota Hull,Mtinko,Singitu na
Mikiwu.
Kwa
upande wao baadhi ya wanafunzi walionufaika mpango huo kutoka shule ya
sekondari Kijota,Hajra Juma alisema mpango huo utawasaidia baadhi ya
wanafunzi walioanza kutumia vipodozi hivyo endapo wataendelea kutumia
vipodozi hivyo.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kijota wakiwa katika viwanja vya
shule hiyo wakiwasikiliza maafisa wa TFDA kutoka Kanda ya Kati
walipokuwa wakitoa elimu juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya
vipodozi vyenye viambato vyenye sumu.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...