Na, Editha Edward-Tabora

Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Bilali Khamis (61) mkazi wa Mtaa wa Ushirika Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora amekatwa sehemu zake za siri na Mpenzi wake Veronica Ngayawula baada ya Kutompa fedha ya sikukuu ya Pasaka hali iliyopelekea kufanyiwa ukatili huo wa kijinsia

Tukio hili la kikatili limetokea majira ya saa saba usiku wa kuamkia tarehe 22 mwaka huu nyumbani kwa Bilali Khamis 

Juma Maswezi ambaye ni ndugu wa Bilali ameiambia Michuzi Blog kuwa kitendo alichofanyiwa ndugu yake siyo kitu kizuri kwani ni uzalilishaji ulio kinyume na haki za binadamu

George Mgalega ni Mganga Mkuu mfawidhi Hospitali ya Wilaya amesema kuwa amekili kumpokea mgonjwa huyo
"Baada ya kumfanyia uchunguzi tumegundua kwamba ametendewa kitendo hicho kwa kutumia kitu ncha kali kwa hiyo afya yake itachukua muda mrefu sana kuimalika maana  kidonda hiki kimekaa wazi kwa muda mrefu"amesema Mgalega 

Hata hivyo kwa matibabu    na uchunguzi zaidi mzee Bilali amepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Nkiga Igunga huku Mpenzi wake Veronica  Ngayawula akiwa ametokomea kusiko julikana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...