Na Humphrey Shao, Michuzi TV
Jopo la Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili lililokuwa likimfanyia Uchunguzi Mwanadada Mariamu Rajabu kuhusu kidonda chake cha Mgongoni limekubalina kwa pamoja kumuamishia mgonjwa huyo katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ibrahim Mkoma amesema kuwa mara baada ya jopo la madaktari wa Hospitali ya Tiafa Muhimbili kufanya uchunguzi kwa kina wameamua kumpa rufani mgonjwa huyo kwenda hospitali ya Ocean Road hili aweze kupata matibabu zaidi.
Hata hivyo waandishi wa habari walipohoji nini matokeo ya uchunguzi wa na kwanini wanamuamishia katika Hospitali ya Saratani Dk Mkoma alikataa kutoa taarifa ya matokeo ya uchunguzi wake na kusema kuwa matokeo hayo ya ugonjwa huo ni siri ya Daktari na Mgonjwa kama kanuni za kitabibu zinavyohitaji.
Hata hivyo Globu ya Jamii ilipomuuliza Mariamu Rajabu juu ya ugonjwa wake alisema kuwa awezi kuzungumzia ugonjwa huo kwa sasa na hayupo tayari kuzungumzia ugonjwa wake.
Muhimbili (MNH) ilianza kumfanyia uchunguzi Mariam Rajab
kubaini chanzo cha kidonda alichonacho mgongoni.
Taarifa za ugonjwa wa Mariam zilisambaa siku chache zilizopita kwenye mitandao ya
kijamii zikimuonyesha binti huyo akiomba msaada wa matibabu kufuatia kidonda
hicho kilichodumu kwa muda mrefu.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha akizungumza na waandishi wa habari amesema hospitali hiyo imechukua
jukumu la kumtibia Mariam baada ya kupata maelekezo kutoka wizara ya afya na
serikali itabeba gharama zote.
Alisema waliona ile video nakufanya juhudi za kumtafuta na hatimaye ametoka Singida na kukaa naye wodini, kwa matibabu yanaendelea na tayari madaktari wamechukua vipimo kwa
ajili ya uchunguzi zaidi.
Mariam alieleza kuwa kidonda hicho amekuwa nacho
kwa muda mrefu na amekuwa akikitibia mara kwa mara ila Agosti 2018 kimefuka
upya na kumsababishia maumivu makali. Mkuu wa idara ya upasuaji MNH, Ibrahim Mkoma amesema matokeo ya vipimo
vilivyochukuliwa ndiyo yatakayotoa mwongozo ni aina gani ya matibabu ambayo
Mariam anatakiwa kupatiw
Jopo la Madaktari waliokuwa wakimuhudumia Mwanadada Mariamu Rajabu aliyelala kwenye kitanda katika hospitali ya Tiafa Muhimbili.
Mwanadada Mariamu Rajabu akiwa amelala kwenye kitanda akisaidiwa na muhudumu wa afya katika hospitali ya Tiafa Muhimbili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...