Na Rhoda Ezekiel, Kigoma

VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)wilayani Kibondo mkoani Kigoma wametakiwa kuacha kupokea rushwa kwa baadhi ya viongozi wanaotaka kwenda kugombea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Serikali Kuu.

Rai hiyo ilitolewa juzi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa Chama hicho kwa ngazi ya tawi, kata na jumuiya hasa namna gani ya kuongoza ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Louis Bura  aliwataka kuwaacha wananchi kuchagua kiongozi aliebora na si kumpendekeza kiongozi ambae amepita na kuwagawia rushwa katika kata zao.

Alisema Katika kuelekea uchaguzi mwaka huu na mwaka 2020 ni lazima viongozi wa chama wanakuwa makini na viongozi wanaotaka Kugombea kwa kuwa watapita mitaani kuwashawishi kwa kuwa wao ndio wapiga kura wa kwanza , na kuwataka viongozi hao kuacha kuchochea kiongozi furani apitishwe kwakuwa katoa hela kiongozi mtoa rushwa hafai katika uchaguzi huu kwa kuwa anakuwa ana lengo lq kuja kujitengenezea masilah yake binafsi.

"Tunafahamu wapo baadhi ya watu wanaotaka kugombea wanapita wanawashawishi muwachague niseme tu kwa yeyote tutakae mkamata hatutasita kumuadhibu na ikiwezekana tutashirikiana na viongozi wa chama kumfuta kabisa katika watu wanaogombea hatutaki viongozi wanaotoa rushwa kiongozi apite kwa kujiamini mwenyewe na kuaminiwa na Wananchi", alisema Bura.

Akiwakaribisha watoa mada walioandaliwa Katibu Wa CCM Wilaya ya Kibondo Stanley Mkandawile aliwataka viongozi wa matawi na kata kuwa wakweli kutoa tathimini za kweli ni mgombea gani anakubalika na  Wananchi ilikuhakikisha  wanakipatia ushindi wa kutosha chama.

Alisema viongozi wanaotoa fedha kuwashawishi wapiga kura kuwachagua hawafai na viongozi ambao hawakubaliki kwa Wananchi hawafai lazima viongozi wa chama wa kata na matawi, kupita kwa Wananchi kujua ni kata gani Chama kina mgombea ambae anakubalika na kata gani ambako kunachangamoto kiongozi aliepo hakubaliki.

Aidha Mkandawile alisema lengo la chama ni kuhakikisha kata 19 na vijiji vyote vya kata hizo wanapata ushindi pamoja ilikufanikisha hilo ni lazima  viongozi kupata idadi ya Wanachama waliopo katika kata zao na kutatua kero zote ambazo zinaweza kusababusha Chama kukosa ushindi.

Katibu Kata ya Misezero Benjamini  Mlinjie  alisema Semina ya kuwajengea uwezo imeweza kuwafungua  fikira za uongozi na mpaka sasa wamejipanga kushirikiana na TAKUKURU  kuwafichua wale wote wasiojiamini na wanataka kutoa rushwa iliwapitishwe.

Alisema wapo baadhi wanatabia hizo na kwa sasa Watahakikisha viongozi wote wanaopita wanauwezo wa kuongoza na Wanapita kutokana na Wananchi wanavyo wakubali na sio kwasababu ya kutoa rushwa.

Alisem wako tayari kumuunga Mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa kuhakikisha chama kinapata viongozi waadilifu na wanaokubalika na Wananchi kwa kuwa chama kinahazina ya kutosha.
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Louis Bura akizungumza na Viongozi wa CCM Wa Wilaya ya Kibondo
 Katibu Wa CCM Wilaya ya Kibondo Stanley Mkandawile akiwakaribisha watoa mada walioandaliwa huku akiwataka viongozi wa matawi na kata kuwa wakweli kutoa tathimini za kweli ni mgombea gani anakubalika na  Wananchi ili kuhakikisha  wanakipatia ushindi wa kutosha chama chao.
 Baadhi ya Viongozi wa CCM Wilaya ya Kibondo Wakiwa katika Semina ya kujengewa uwezo wa uongozi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...