Mwanasheria
mkuu wa kwanza Tanzania Jaji Mstaafu Mark Bomani amewataka watanzania
kuchangamkia fursa ya mabadiliko ya sheria katika sekta za maliasili na
madini yaliyofanyika hivi karibuni,kutokana na sheria hizo kuweka
mazingira ya usawa (win - win situation)tofauti na sheria zilizokuwepo
awali kutoa kipaumbele kwa wawekezaji kutoka Nje ya nchi.
Jji Mstaafu Mark Bomani ameyasema hayo alipomtembelea ofisini kwake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusu sekta ya madini nchini na kuongeza kuwa Tanzania ina utajiri mkubwa wa madini unaotosha kuendesha Nchi ukiachilia mbali maliasili nyingine zilizopo tatizo ni kuwa madini hayo hayakulinufaisha Taifa.
“Mabadiliko ya sheria waliyoyafanya yatasaidia sana,sasa ni jukumu letu sisi Watanzania kuichangamkia fursa hiyo na tusisubiri kulalamika kama ilivyo kawaida yetu,tfanye kazi kwa bidii maana utajiri huu wa madini tuutumie na kujiletea maendeleo binafsi na yanchi kwa ujumla kwa kuwa sasa sheria hizi mpya zimeweka uwanja sawa”
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi mbali na kumshukuru Jaji Mstaafu Mark Bomani kumtembelea ofisini kwake ameongeza kuwa mabadiliko yaliyofanyika katika sheria za madini yametokana kwa kiasi kikubwa na ripoti ya tume iliyoundwa kuchunguza sekta ya madini ikiongozwa na Jaji Mstaafu Mark Bomani.
“Haya yoote tuliyoyabaini na kuyaeleza kama upungufu yamo kwenye ripoti ya Bomani ingawa kuna mengine tuliyoyaongeza kama vile mrahaba ulio chini,kutolipa kodi na mengine mengi na kwakuwa Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameutangaza mwaka 2019 kuwa mwaka wa uwekezaji,Mzee Bomani amekuja ili tubadilishane mawazo tuone namna ya kuuboresha mwaka huu wa uwekezaji”

Ameongeza
kuwa wamezungumzia namna ya kuweka mikakati ya kuwavutia wawekezaji
wenye tija kuja nchini kuwekeza ili Taifa liweze kunufaika na madini
kupitia kodi,ajira kwa vijana na kwamba ujio wa Jaji Mstaafu Mark Bomani
ofisini kwake umemjengea ari na nia ya kuonana na viongozi wengine
waliolitumikia Taifa kwa tija ili aweze kupata maoni yao ya namna ya
kuendesha shughuli za serikali katika wizara aliyopangiwa kazi na Rais
Dkt John Pombe Magufuli.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (kushoto) akimsikiliza kwa
makini mgeni wake Jaji Mstaafu Mark Bomani alipomtembelea ofisini kwake
jijini Dar es salaam.
PICHA 2: Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba
John Kabudi (kushoto) akiwa na mgeni wake Jaji Mstaafu Mark Bomani
alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es salaam.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...