Na Shushu Joel,Mkuranga.

NAIBU waziri wa mifugo na  uvuvi na mbunge wa jimbo la Mkuranga mkoani Pwani AbdAllah Ulega amewatembelea wahanga  waliokumbwa na majanga ya kubomoka kwa nyumba zao na kupelekea kupata hifadhi kwa wasamalia wema.

Akizungumza na wananchi hao  Ulega aliwapa pole na kuwaomba kuendelea kuwa na subra wakati serikali  ya awamu ya tano ikifanya tathimini ili kubaini kaya zote zilizokumbwa na majanga hayo.

Aliongeza  kuwa majanga kama haya si  ya kisiasa bali yanapangwa na Mungu hivyo katika kipindi hiki  kigumu kwa wananchi wa vikindu ambao ndio waathirika wakubwa wanapaswa kuendelea kuwa watulivu.

Aidha alisema kuwa taarifa za awali alizozipata kuhusu kaya zilizokumbwa na majanga hayo zilikuwa ni 100 lakini kufikia jioni ziliongezeka mpaka kufikia kaya 178 ,ni kaya nyingi kwa kweli kwani wananchi hao wanapata changamoto  kwa sasa.

Pia Naibu waziri huyo amewapatia pole wananchi hao zilizotolewa na Rais wa jamhuri  ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kusema anatambua kilichotokea katika jimbo la Mkuranga na kuwataka  kuzidisha maombi ili Mungu awaondolee majanga.

Aidha katika ziara hiyo ya kuwatembelea wahanga hao Ulega ametembelea familia iliyopoteza mama na mtoto  kwa kuuwawa kwa radi.
"Ofisi ya mbunge imetoa kiasi cha zaidi ya milioni 3 ili kusaidia baadhi ya wahanga wa nyumba zilizoezuliwa na  upepo mkali na itaendelea kuwasaidia  ili kuhakikisha kila  mmoja anarudi kwenye nyumba yake na kuendelea na shughuli zake za uzalishaji"Alisema Ulega.

Kwa upande  wake shuhuda wa tukio hilo,Juma Said  alisema  kuwa radi iliposhuka katika maeneo hayo hali ya hewa kama ilibadirika yote mama wa familia hiyo alikuwa nje ghafla alianguka na huku vijana waliokuwa ndani walipiga kelele ndio tuliwai kutoa msaada kwa mama huyo kimkimbiza hospital ila kijana alikuwa ameshakwisha kufariki.
Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi  mbunge  wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega   akiwapa pole wanafamilia  waliokumbwa na majanga ya kubomoka kwa nyumba zao na kupelekea kupata hifadhi kwa wasamalia wema.
Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi  mbunge  wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega   akiwapa pole wanafamilia  waliokumbwa na majanga ya kubomoka kwa nyumba zao na kupelekea kupata hifadhi kwa wasamalia wema.
Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi  mbunge  wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega   kulia akiwa amekaa na wafiwa katika msiba , ambapo aliwafariki na kuwaomba kuendelea kuwa na subra  katika kipindi hiki  kigumu ,Wananchi wa vikindu ambao ndio waathirika wakubwa wanapaswa kuendelea kuwa watulivu.


Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi  mbunge  wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega akimsikiliza mmoja wa wananchi ambae nyumba yake ilikumbwa na majanga ya kubomoka na kupelekea kupata hifadhi kwa wasamalia wema.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...