* Atoa milioni kumi kuendesha ofisi za wajane na kuhaidi kujenga ofisi za wajane makao makuu Dar

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa atachukua takwimu za matatizo ya wajane wa Mkoa  huo na kumkabidhi Waziri wa Sheria na Katiba ambaye atamkabidhi jaji Mkuu  ili matatizo hayo yaweze kushughulikiwa ndani ya miezi mitatu.

Akizungumza katika kongamano lililolenga kutatua kero za wajane katika masuala ya mirathi, uchumi na malezi Makonda amesema kuwa baada ya kukutana na wanawake na watoto waliotelekezwa mwaka uliopita  matatizo mengi zaidi yaligundulika na kumpa uthubutu wa kuendelea mbele zaidi.

Amesema kuwa moja ya kitu wanachotarajia ni pamoja na kuweka mifumo bora na endelevu ya uongozi ili kuviepusha vizazi vijavyo na matatizo haya yanayojitokeza sasa.

Amesema kupitia kongamano hilo ataangalia mfumo wa sheria ambao utawasaidia wao na wengine huko mbeleni huku akisema katika suala la uchumi lazima akina mama hao watambue haki yao ya asilimia 4 ya fedha iliyotengwa na Serikali ambayo hutolewa bila riba na katika  sekta ya malezi Makonda amesema kuwa  kuna wataalamu watakaoshirikiana nao katika kupata ushauri juu ya namna bora ya kuwalea watoto wao ambao wengi wameharibikiwa kutokana na maendelea ya sayansi na teknolojia hasa katika mitandao ya kijamii.

Kwa upande wake katibu tawala wa Mkoa Abubakar Kunenge amewashukuru akina mama hao pamoja na wawezeshaji  kwa kujitokeza kwa wingi huku akitoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kwa kuandaa kongamano hilo ambalo limelenga kutatua kero za mirathi,uchumi na malezi.

Akisoma taarifa   Mwenyekiti wa kamati ya kuwasaidia watoto na wanawake wanaoishi kwenye mazingira magumu ambaye ni wakili wa kujitegemea na mshauri msaidizi wa masuala ya kisheria wa CCM Albert Msando amesema kuwa matokeo ya kampeni iliyoanzishwa na mkuu wa Mkoa iliyolenga kuwasaidia watoto na wanawake wanaoishi kwenye mazingira magumu  wengi wa wazazi wa watoto hao ndio hao wajane waliojitokeza leo katika kongamano hilo, na amesema kuwa kamati hiyo ya watu 19 imegundua matatizo mengi kwa watoto hao ikiwemo kubakwa, kukosa haki za msingi, kunyanyaswa na kudhulumiwa huku utatuzi wa changamoto hiyo ni kubwa kuliko matatizo mengine.

Kwa upande mchungaji wa kanisa Anglican Mchungaji Daniel  Mgogo amesema kuwa mamia wa wajane hao wamedhulumiwa na amewashauri viongozi wa Serikali kuanzia ngazi ya kata kusikiliza kero za aina hiyo huku akimpongeza Mkuu wa Mkoa kwa hekima na uthubutu huo aliouonesha katika kuwasaidia wajane hao na kushauri kuwa suala la mirathi liwe sheria kwa kila mmoja kuandika mali na warithi wake ili kuwalinda wajane.

Kongamano hilo limehudhuriwa na wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam, wasanii, wanasaikolojia, wawezeshaji, wanasheria pamoja na asasi 9 zisizo za kiserikali ambazo zimeshiriki katika kuwasaidia wajane hao kupata haki zao za kisheria kupitia kongamano hilo.
 Mwimbaji wa taarabu Khadija Kopa akifurahi pamoja na akina mama  wajane walioitikia mwito wa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda katika kongamano la utatuzi wa masuala ya mirathi, uchumi na malezi, leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wajane waliohudhuria kongamano hilo la utatuzi wa masuala ya mirathi, uchumi na malezi lililoandaliwa na  mkuu wa Dar es salaam Paul Makonda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...