Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, inawahamasisha Watanzania wenye sifa kuomba nafasi ya ajira katika Jumuiya ya Madola, London, Uingereza.
Nafasi hiyo ni Afisa Rasilimali Watu Msaidizi atakayefanya kazi katika kitengo cha Rasilimali Watu na Usimamizi wa Miundombinu. Taarifa zote muhimu kuhusu fursa hiyo ya ajira zinapatikana kwa kupitia tovuti http://thecommonwealth.org.jobs.
Kwa kuzingatia sera ya Jumuiya ya Madola ya usawa wa kijinsia, Sekretarieti ya taasisi hiyo inawahimiza wanawake wengi zaidi wenye vigezo kuomba nafasi hizo. Mchakato wa kumpitisha mtaradhia wa nafasi hiyo utazingatia uwiano wa kikanda hususan kwa nafasi za maafisa waandamizi.
Mwisho wa kutuma maombi kwa nafasi hizo ni Ijumaa tarehe 12 Aprili, 2019.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma
4 Aprili, 2019.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...