Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka kuhakikisha inaandaa wote wanaotarajiwa kutoa ushahidi wao dhidi ya kesi ya vigogo wa Simba ambayo itasikilizwa kwa siku tatu mfululizo, mwezi ujao.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, Makamu wake, Geofrey Nyange maarufu kwa jina la Kaburu na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Takukuru,Leonard Swai kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini mshtakiww Aveva hayupo.

Hakimu Simba amesema shauri hilo litakapokuja tena mahakamani hapo tunawahitaji mashahidi wote waliobaki kufika kwa ajili ya kutoa ushahid. " Upande wa mashtaka tunategemea mtatuletea mashahidi wote waliobaki ambao nataka watoe ushahidi kwa siku tatu mfululizo,"amesema Simba.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 13 kwa ajili ya kutajwa na itasikilizwa Mei, 15, 16 na 17 mwaka huu.

Katika kesi hiyo Hans Poppe anakabiliwa na mashtaka mawili ya kughushi nyaraka na kuwasilisha nyaraka za uwongo yeye pamoja na wenzake.

Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka mengine zaidi ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kuhamisha fedha hizo bila mamlaka ya Kamati ya Utendaji ya Simba, kujipatia pesa isivyo halali (Aveva) na utakayishaji fedha yanayowakabili wote, Aveva na Kaburu.

Katika maelezo ya awali, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa Machi 12, 2016, Klabu ya Simba ililipwa jumla ya Dola za kimarekani 319, 212 na Klabu ya Etoile Sportive Du Sahel ya nchini Tunisia.

Kiasi hicho cha fedha kilikuwa ni ada ya uhamisho wa mchezaji Emmanuel Okwi kwenda Klabu ya Etoile Sportive Du Sahel ya nchini Tunisia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...