Waziri
Nchi,Ofisi yaMakamu wa Rais, Anayeshughulikia Mazingira na Muungano
Mhe.January Makamba akizungumza katika mkutano wa Mabadiliko ya
Tabianchi uliofanyika leo jijini Dodoma katika ukumbi wa hotel ya Morena
Na.Vero Ignatus ,Dodoma
Mkutano
mkuu wa Mabadiliko ya Tabianchi umefanyika leo Jijini Dodoma
ukiwashirikisha wadau zaidi ya 100 wameshiriki katika mkutano huo ukiwa
na lengo la kujadili mabadiliko ya Tabia nchi na kujikwamua katika taizo
hilo kama Taifa
Akifungua
mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa FORUMCC Eric Mugurusi amesema lengo kuu
la mkutano huo ni kujadili Sera ambazo zitatilia maanani mabadiliko ya
Tabia nchi na namna ambavyo wananchi watashirikishwa ili kupunguza
athari za mabadiliko hayo.
Amesema
kuwa mkutano huo ni maalum kwaajili ya kuona nam,na ambavyo sera
zinavyoweza kuwaondoa kwenye tatizo hiolo na ushirikiswahwaji wa
wananchi katika hayo yote.
Waziri
Nchi,Ofisi yaMakamu wa Rais, Anayeshughulikia Mazingira na Muungano
Mhe.January Makamba akizungumza katika mkutano wa Mabadiliko ya
Tabianchi amesema katika kuhakikisha tunaondoa tatizo la mabadiliko ya tabia nchi kuwajumuishe
watu wote, kujifunze katika nchi zilizofanikiwa na kuzitumie mbinu
hizo, Kuaanda Sera nzuri,Kuwahimiza watunga Sera kuamuru uchukuliwaji wa
hatua
Mhe.Makamba
amesema kuwa kwenye baadhi ya nchi Mabadiliko ya tabia ya nchi
yametangazwa kama usalama wa nchi ambapio nasi kama nchi ipo haja ya
kuonesha kuwa changamoto zinaweza kuwa kubwa kwani Utalii wetu ni Fukwe
ambazo zinalika na thamani yake inaondoka sababu ya mabadiliko ya tabia
ya nchi,hivyo utalii unapotea.
"Mama
yangu alikuwa Nesi miaka ya 1980 anasema kipindi hiko hakukuwa kabisa
na kesi za wagonjwa wa malaria, lakini angali miaka ya sasa,Wagonjwa wa
malaria wamekuwa wengi na ndo ugonjwa mkubwa hii ni sababu ya ongezeko
la Mbu kwa kasi kubwa na kutokutunza mazingira yetu”Alisema Makamba
Amesema
kati ya miaka 5-10 mabadiliko ya tabia nchi yalionekana kama nadharia
au yanawahusu wanasayansi ila kadri siku zinavyozidi kwenda ndivbyo
tatizo linavyozidi kuwa kubwa, hata kwenye kilimo sababu ya mabadiliko
ya Majira kumesababisha kuchelewa kwa mvua hivyo Kilimo kinafanyika kwa
shida pia yanapelekea umasikini.
Mimi nilisomeshwa sana kwa kilimo cha Chai na Kahawa ambacho ndio kikubwa Tanga, lakini sasa hivi kilimo cha mazao haya kinapotea,hali hii ni ishara ya kuongezeka kwa umasikini''Alisema Makamba
Kwa upande wake Meneja Mradi kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Oxfam Jovita Mlay amesema kuwa Mabadiliko ya Tabianchi yanaongeza umasikini kwa wanawaume na wanawake lakini wahanga wakubwa zaidi ni wakina mama na watoto kwani inagusa maeneo ambayo wanawake wanajipoatia kipato napo no kwenye kilimo.
Amesema
kuwa wakati wa kushughulikia majanga kama hayo ni muhimu kuhakikisha
kuwa inawekwa mipango na usimamizi wa kisera unaoweza kupunguza na
kumaliza madhara ya yatokanayo na mabadiliko ya Tabianchi kwa
kuwashirikisha wadau mbalimbali
Amesema
Oxfam inaendelea kufanya kazi ili kuhakikisha kuwa maswala
yanayoingizwa katika mipango mikakati na kuendelea kusapoti juhudi
zinazofanywa na wadau katika kupambana na mabadiliko ya Tabianchi.
Kwa
upande wake mbunge wa Babati vijijini Mhe,Jitu Soni amesema kuwa jamii
nyingi zinaishi katika mazingira magumu kutokana na mabadiliko ya
Tabianchi amesema kuwa mabadiliko hayo siyo jambo la mazingira peke yake
bali linahusisha maswaka ya uchumi,miundombinu,mifumo ya
uzalishaji,rasilimali,na nishati.
Nae
Mwenyekiti wa Bunge ya Bajeti na mbunge wa Kibakwe Mhe.George
Simbachawene amesema kuwa mgawanyo wa shughuli za kibinadamu imekuwa
sababu kubwa ya uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya
Tabianchi,amesema bado elimu inahitajika zaidi katika jamii zetu haswa
vijijini ili kujinasua katika tatizo hilo.
Aidha watu wengi wanaharibu mazingira kwasababu ya kutafuta maji na nishati,uwekezaji wa kutafuta maji unatumia gharama kubwa sana,amesema nchi inahitaji kutengeneza mfumo wa kitaalam katika uharibifu wa mazingira kwani hali ni mbaya sana
Mshiriki
kutoka Asasi za kiraia mkoa wa Kagera bi Zainabu Shakiru amewaomba
Serikali pamoja na wadau kuwa mchakato wa utekelezaji wa sera ya
mabadiliko ya tabianchi wananchi nao washirikishwe ipasavyo ili waweze
na wao kuitambua sera hiyo
Washiriki wa mkutano wa tano wa mabadiliko ya Tabianchi Jijini Dodoma leo
Ndugu
Jensen Shuma kutoka shirika la TaTEDO akichangia mada katika mkutano wa
tano wa mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Jijini Dodoma
Dkt.Lucy
Ssendi Mshauri wa Maswala ya Mabadiliko ya Tabianchi ,Mradi wa
Decentralized Climate Finance -TAMISEMI akichangia mada katika mkutano
wa Tano wa mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Jijini Dodoma
Makamu
Balozi wa EU Nchini Tanzania Charles Stuart akizungumza na washiriki wa
mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Jijini Dodoma leo.
Jovita
Mlay Meneja wa Mradi kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Oxfam
Tanzania akizungumza katika mkutano wa mwaka wa mabadiliko ya Tabianchi
uliofanyika leo Jijini Dodoma katika hoteli ya Morena
Washiriki
kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini Tanzania waliohudhuria
katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Jijini Dodoma
katika Hotel ya Morena.
Mkurugenzi
mtendaji wa Jumuiko la maliasili Tanzania( TNRF)Zakaria Faustin
akizungumza katika mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Jijini
Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...