Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
FAILUNA Abdi Matanga kutoka Tanzania ameshika nafasi ya tatu  katika mbio za Hispa Hambarg marathoni kwa upande wa wa wanawake mashindano yaliyomalizika leo mchana nchini Ujerumani na kuvunja rekodi ya muda wake wa awali.

Failuna amekimbia kwa muda wa saa 2:27:56 na kutunukiwa medali ya shaba huku mkimbiaji mwingine kutoka Tanzania Gloria Makula akishiaka nafasi ya 30 baada ya kukimbia kwa muda wa 2:49:07.

Failuna aliachwa kwa muda wa dakika tatu na mshindi wa medali ya dhahabu wa mbio hizo Dibabe Kuma kutoka nchini Ethiopia ambaye alitumia saa 2:24:42 huku nafasi ya pili ikishikiliwa  Magdalyne Masai kutoka Kenya aliyekimbia kwa saa 2:26:04.

Kupitia ujumbe wa Whatsap Failuna amesema kuwa alitamani kushinda medali ya dhahabu lakini alipitwa dakika za mwishoni.

Katika mashindano hayo kwa upande wa wanaume Tadu Abate  kutoka Ethiopia ameshinda baada ya kukimbia kwa saa 2:08:26 huku raia mwingine kutoka Ethiopia Ayele Abshero akimaliza nafasi ya pili kwa kutumia saa 2: 08:27 wakimwacha mshindi na bingwa wa Olympiki wa mwaka 2012 Stephen Kiprotich kutoka Uganda aliyeshika nafasi ya tatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...