Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akikagua mlango (geti) la kielektroniki kwa ajili ya ukaguzi wa abiria,
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA Aprili 27, 2019.(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifurahia jambo na Watalii kutoka Israel, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA, kutoka kushoto ni Naomi Moscovich, akiwa na binti zake, Dana Moscovich(kulia) na Lihi Moscovich (katikati). Aprili 27, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
…………………………………………………………………….
*Ni yenye kuonyesha wanyama, milima, fukwe, mambo ya utamaduni
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ameuagiza uongozi wa bodi ya KADCO uhakikishe unaweka mabango ya
kielektroniki yenye kuonesha vivutio vya utalii kwenye uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
“KADCO na Wizara ya Maliasili na
Utalii, shirikianeni kuweka utaratibu wa kutangaza vivutio vyetu vya
utalii hasa wanyama kwenye viwanja vyote vya ndege. Tunazo mbuga,
milima, fukwe za bahari na ngoma za makabila mbalimbali, wekeni mabango
yanayobadilisha picha.”
“Screens zenye wanyama
wanaobadilikabadilika zinaleta mvuto lakini pia ni fursa ya kutangaza
vivutio vyetu. Nimezunguka humu ndani, kuta zote ni nyeupe tu, tumieni
fursa hiyo kutangaza tamaduni zetu na vivutio tulivyonavyo,” Waziri Mkuu
alimweleza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kilimanjaro Airports
Development Company (KADCO), Mhandisi Christopher Mukoma.
Alitoa agizo hilo jana mchana
(Jumamosi, Aprili 27, 2019) wakati akikagua miundombinu ya uwanja wa
ndege wa Kilimanjaro (KIA) mara baada ya kuwaaga watalii 274 kutoka
Israeli wanaowawakilisha wenzao 1,000 walioondoka nchini jana kurejea
kwao.
Akiwa uwanjani hapo, Waziri Mkuu
alikagua eneo la mapokezi, sehemu ya abiria wanaoondoka na wanaowasili,
sehemu ya uhamiaji, mashine za kukagua mizigo ya wanaoondoka na
wanaowasili, sehemu za kutolea huduma na maduka.
Pia alimwagiza Mrakibu
Mwandamizi wa Uhamiaji kwenye kiwanja hicho cha ndege, Bw. Filbert Ndege
awasiliane na makao makuu yake ili waangalie uwezekano wa kuongeza
madirisha ya kutolea huduma za uhamiaji (counters) ili huduma hiyo
itolewe kwa kasi zaidi.
“Angalieni cha kufanya, ikibidi eneo hili lipanuliwe na counters nyingine ziongezwe ili kufast–track utoaji wa huduma hasa msimu ambao watalii wengi huingia nchini.”
Pia aliwataka KADCO waboreshe
eneo la maegesho ya magari kwa kufanya upanuzi na kujenga maturubai ya
vivuli (shades) ili kuyakinga na jua kali magari ya wateja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...