Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe, Mhandisi Atashasta Nditiye afungua rasmi Baraza jipya la wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania - TRC katika ukumbi wa Bandari jijini Dar es Salaam hivi karibuni Aprili 2019.                                                        




Hafla hiyo ya ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi TRC kwa mara ya kwanza 
tangu kuunganishwa kwa iliyokuwa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL na Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli – RAHCO na kuanzishwa TRC.

Baraza jipya la wafanyakazi lina jukumu la kusimamia na kutetea maslahi ya wafanyakazi kupitia wawakilishi kutoka idara na vitengo vya taasisi pamoja na wajumbe wa kamati tendaji wanaotokana na wajumbe wa baraza.

kulingana na katiba ya baraza na taratibu za kisheria Baraza lina kazi ya kupitia na kutoa maoni na kuboresha utendaji wa Shirika,pia baraza ni chombo cha kuleta upendo na umoja baina ya wafanyakazi. 

Mgeni rasmi wa ufunguzi wa Baraza hilo naibu waziri Mhe. Atashasta Nditiye amelipongeza Shirika la Reli Tanzania kwa kufanya uamuzi huo wa kuundwa Baraza jipya na kuwataka wajumbe kulifanya Baraza kama sehemu wa kuwawakilisha wafanyakazi kwa lengo la kutatua matatizo changamoto na kuleta tija katika Shirika. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania - TRC alisema kuwa serikali inafuatilia Mali za Shirika ambazo zinamilikiwa na watu binafsi wamejibinafisha kwa njia zisizo halali na kuomba wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania kushirikiana katika kutoa taarifa sahihi ili rasilimali hizo zirudi kuongeza mapato kusaidia kuendesha Shirika ikiwemo kuinua maslahi ya wafanyakazi.


Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe, Mhandisi Atashasta Nditiye akifungua rasmi Baraza jipya la wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania - TRC katika ukumbi wa Bandari jijini Dar es Salaam hivi karibuni Aprili 2019.
Picha tofauti za matukio katika Hafla ya ufunguzi wa Baraza la kwanza la wafanyakazi TRC tangu kuunganishwa kwa kampuni mbili zilizokua TRC,yaani Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) na kampuni hodhi ya Reli (RAHCO) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...