Na Joseph Mpangala-Mtwara.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evodius Mmanda amewataka Mananchi waliofika eneo la Uwanja wa Ndege Mkoani Mtwara kwa ajili ya kujihifadhi kuhakikisha wanajiorodhesha katika kitabu cha Kumbukumbu ili kuepuka kupoteana.
Mmanda ameyasema hayo wakati akitembelea maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya kujihifadhi kufuatia tahadhali iliyototelewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA ya kuwepo kwa Kimbunga Keneth ambacho kilitabiriwa kutokea Alhamis Wiki Hii.
Aidha Mmanda amewaomba wananchi hao kuwapa taarifa wenzao ambao wamekaidi kuondoka majumbani mwao na kuelekea maeneo yaliyotajwa.
Maeneo yaliyoandaliwa kwa Mwananchi kujihifadhi ni Shule ya Mitengo,Sabasaba,Uwanja wa Ndege,Naliendele pamoja na Shule ya sekondari ya Sabodo.
Wafanyakazi wa Serikali pamoja na wanafunzi wameagizwa kutokwenda kutokana na Utabiri wa Uwepo wa Kimbunga Keneth siku ya alhamis.
Baadhi ya Wananchii wamekusanyika katika Eneo la Uwanja wa Ndege Mkoani Mtwara kwa Tahadhari ya kujilinda na Kimbunga Kenneth kilichotabiriwa kutokea Leo na Mamlaka ya Hali ha Hewa Tanzania TMA.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara mjini Mh.Evodius Mmanda akizungumza na baadhi ya Wananchi waliokusanyika katika uwanja wa ndege Mkoani Mtwara kwa tahadhari ya kujilinda na Kimbunga Kenneth kilichotabiriwa kutokea leo na Mamlaka ya Hali ha Hewa Tanzania TMA.
Baadhi ya Wananchi wakiwa wamekusanyika kwa pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...