Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akishiriki kubeba matofali wakati wa
ujenzi wa nyumba za askari polisi eneo la Njiro mjini Arusha ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya Sherehe za Muungano.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), Jonathani Shana akimkaribisha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kushiriki ujenzi wa nyumba Sita za
Polisi eneo la Njiro mjiani Arusha jana ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho
ya Sherehe za Muungano.
Askari na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wakishiriki
usaombaji wa matofauri wakati wa ujenzi wa nyumba za makazi kwa askari
hao eneo la Njiro mjini Arusha ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya sherehe
za Muungano.
Askari Polisi wakiwa chini ya msingi kwa ajili ya kumwaga zege wakati wa
ujenzi wa nyumba za askari eneo la Njiro mjini Arusha ikiwa ni sehemu
ya maadhimisho ya sherehe za Muungano.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mwenye jacket akiwa na Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), Jonathan Shana wakishiriki kubeba zege
wakati wa ujenzi wa nyumba za polisi eneo la Njiro mjini Arusha ikiwa ni
sehemu ya sherehe za Muungano.
Askari na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha
wakishiriki usaombaji wa matofauri wakati wa ujenzi wa nyumba za makazi
kwa askari hao eneo la Njiro mjini Arusha ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho
ya sherehe za Muungano.
ASKARI wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wamesheherekea
Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanziba kwa kushiriki ujenzi wa nyumba Sita
za makazi ya askari polisi eneo la Njiro mjini Arusha.
Ujenzi huo uliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mrisho Gambo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana na maofisa wa
polisi mkoani humo walioshiriki kubeba matofali na kumwaga zege kwenye msingi
za nyumba hizo.
Akizungumza eneo la tukio RC Gambo alisema serikali
ya mkoa itaendelea kuhakikisha inaondoa changamoto ya ukosefu wa makazi bora
kwa askari wake hatua itakayowawezesha kufanya kazi kwa utulivu na umakini
zaidi.
Naye Kamanda Shana alimshukuru Rais Dk. John
Magufuli, Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini
(IGP), Simon Nsiro kwa kuendelea kuboresha makazi ya askari mkoani humo.
Ujenzi wa nyumba hizo Sita unatarajiwa kuchukua
familia Sita za watu takribani 5 kwa nyumba na hivyo kufanya kuwa na watu
takribani 30 watakaoishi kwenye nyumba hizo.
|
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...