Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu cha Manispaa ya Kinondoni (KIFA) na  mjumbe wa Chama Cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kwenye mkutano mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Michael Simon Lupiana (72) maarufu kwa jina la Mzee Lupiana (pichani) amefariki Dunia baada ya kugua muda mfupi.
Mtoto wa marehemu, Lupiana Lupiana alisema kuwa baba yake alilazwa Hospitali yaTaifa ya Muhimbili siku ya Ijumaa Kuu akisumbuliwa na shinikizo la damu (Pressure) na Kisukari ambayo yalisababisha matatizo ya figo na kufariki dunia saa 5.30 usiku wa sikukuu ya Pasaka.
Lupiana alisema kuwa msiba kwa sasa upo nyumbani kwao, Kimara Stop Over na wanatarajia kuzika siku ya Jumatano kwenye makaburi ya Kinondoni.
 “Kwa sasa tupo katika harakati za kukamilisha masuala mbalimbali ya msiba wa mpendwa Baba yetu na matarajio ni kumpunzisha katika nyumba yake ya milele siku ya Jumatano kwenye makaburi ya Kinondoni, taratibu nyingine zitatolewa baadaye,” alisema Lupiana.
Hiki kilikuwa kipindi cha pili cha uongozi cha marehemu Mzee Lupiana ambapo mwakani alikuwa anamalizia muda wake.
 Mbali ya kuwa kiongozi wa mpira, marehemu pia alikuwa mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wa wadogowadogo madini ya kujengea (DACOREMA) na aliwahi kuwa diwani wa Kata ya Kinondoni.
Attachments area

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...