Na Ripota Wetu, Musoma
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeamua kuendesha ukaguzi wa kushutukiza katika masoko yaliyopo wilayani Musoma Mjini, mkoani Mara ikiwa ni mwenedelezo wa mkakati wa shirika hilo kuondoa bidhaa ambazo hazina ubora kwenye soko nchini.
Ukaguzi huo umeendeshwa na maofisa wa TBS ambapo ukaguzi huo umekwenda sambamba na kuondoa kwenye soko nguo za ndani za mitumba kutokana na matumizi yake kupigwa marufuku nchini kwa kuwa zina madhara kiafya kwa watumiaji.
Mbali na hatua hiyo, pia sampuli mbalimbali za bidhaa zimechukuliwa katika masoko hayo kwa lengo la kwenda kuzipimwa kwenye maabara za shirika hilo ili kujiridhisha kama zinakidhi viwango, huku vilainishi vya magari visivyokuwa na ubora vikiondolewa kwenye soko, kwenye baadhi ya maeneo ya kanda ya ziwa ambako operesheni hiyo imefanyika.
Akizungumza wakati wa operesheni hiyo Mkaguzi wa TBS, Baraka Bajije, amesema kuwa katika ukaguzi huo unaendelea Kanda ya Ziwa kabla ya Musoma Mjini umefanyika pia masoko maeneo ya Mwanza Mjini, Sengerema, Magu, Bunda na sasa Musoma Mjini ambapo wamefanikiwa kukamata shehena ya nguo za ndani za mitumba pamoja na taulo zinazokadiriwa kuwa na thamani ya Sh. milioni 10.
Amesema kuwa Sheria ya Viwango Namba 2 ya mwaka 2009 inazuia matumizi ya nguo za ndani za mitumba pamoja na taulo, lakini bado watu wasiowaaminifu wamekuwa wakiziingiza kwenye soko la Tanzania kupitia njia za panya.
Pia Bajije amesema bidhaa hizo haziruhusiwi kabisa kuwepo sokoni kutokana na madhara yake kwa watumiaji ikiwemo kusababisha magonjwa sugu ya fangasi, kansa ya ngozi na magonjwa mengine.
Ametoa mwito kwa Watanzania kuacha kabisa kutumia nguo hizo kutokana na madhara yake kuwa makubwa.Wakizungumza wakati wa operesheni hiyo baadhi ya wananchi wameunga mkono hatua zinazochukuliwa na TBS kuondoa sokoni nguo hizo. "Nguo hizi za ndani za mtumba watu
tulikuwa tunazipenda kwa sababu uimara na unafuu wa bei, lakini baada ya kuelimishwa madhara yake na TBS, lazima na sisi Watanzania tubadilike," amesema Joyce Magesa.
"Leo hii watu wanapenda kuzinunua kwa kuvutiwa na bei ya Sh. 1,000 kwa sidiria, lakini ukipata kansa ya matiti gharama za kujitibia hazilingani kiasi hicho cha fedha.Nikiri wanawake walio wengi ndio watumiaji wa kubwa ikilinganishwa na wanaume,lakini elimu tunayoendelea kuipata kutoka TBS itatusaidia kuachana na uvaaji wa nguo za ndani ambazo ni za mtumba,"amesema.
Imefafanuliwa nguo za ndani zilizopigwa marufuku ni pamoja na soksi, taiti, sidiria, taulo na nyingine. Wakati huo huo TBS inaendesha operesheni ya ukaguzi wa bidhaa sokoni ili kubaini bidhaa zisizo na viwango zilizopo humo. Kwa sasa maofisa wa shirika hilo wapo mikoa ya kanda ya ziwa wakiendesha uendesha msako huo wa bidhaa hafifu sokoni.

Sehemu
ya shehena ya nguo za mitumba zikiwa zimekamatwa kwenye masoko
mbalimbali ya Musoma Mjini baada ya maofisa wa Shirika la Viwango
Tanzania(TBS) kufanya msako wa kushtukiza
Taulo
ambazo zimeshutumika maarufu taulo za mtumba zikiwa zimeshikiliwa na
maofisa wa TBS baada ya kuzikamata katika masoko ya wilayani Musoma
Mjini baada ya kufanya msako mkali
Nguo
za mitumba zikipakiwa kwenye gari baada ya kukamatwa na maofisa wa
Shirika la Viwango Tanzania(TBS)waliopo mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo
wanaendelea na msako wa kushtukiza katika masoko kwa lengo la kuondoa
bidjaa zisizokuwa na ubora pamoja na nguo za mitumba

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...