SHIRIKA la reli  nchini limewatoa hofu watanzania kuhusu umeme Utakao tumika katika shughuli zote za kuendesha usafiri wa treni ya  umeme inayotarajiwa kuanza kazi zake za usafiri tokea  Dar es Salaam mpaka Morogoro kwa hatua ya kwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa mradi kutoka Dar es Salaam mpaka  Morogoro  Eng  Ayubu Mdachi alisema kuwa  kukamilika kwa reli hiyo kutaongeza pato kubwa kwa taifa.
Aidha  amewataka wananchi kuwa walinzi wakuu wa mradi huo kwani kuna watu wengine  hawana  nia njema na maendeleo ya nchi yetu.
Aliongeza  kuwa umeme utakaotumika  katika uendeshaji wa treni  hiyo ni wa hali ya juu kwani kila  mkoa utakuwa umeunganishwa hivyo kama ikitokea kukatika kwa umeme Morogoro basi treni hiyo itatumia wa mkoa wa pwani la sivyo ukatike  nchini nzima napo  bado  treni hiyo itafanya kazi zake kutokana  na uwezo wake wa kutunza umeme yenyewe.
Kwa upande wake Edwini  Kalisa katibu wa baraza la wafanyakazi  la shirika  la reli nchini alisema kuwa serikali  inasitahili pongezi za dhati  kutokana na hali halisi  jinsi inavyoelekea katika nchini yetu kwani mizigo itasafirishwa kwa urahisi na haraka kuliko Barabara  za kupitia magari.
 Aliongeza kuwa usafirishaji  wa treni ijayo ya umeme itasaidia sana kwenye sekta ya viwanda kutokana na uwepo  wa malighafi kutegemeana kutoka sehemu  mbalimbali za mkoa.
Aidha katibu huyo aliongeza kuwa treni hiyo itakuwa  ni ya kwanza barani  Afrika kutokana na ubora wake unavyoonekana.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi  la Shirika  la reli nchini,Edwini  Kalisa akizungumza leo  na waandishi wa habari  katika kituo cha soga mara baada ya kutembelea na kukagua jinsi mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa standard Gauge Soga mkoa  Pwani.(Picha na Emmanule Massaka wa Mchuzi TV Dar es Salaam)
Meneja Msaidizi  SGR kwa upande wa Shirika la Reli nchini(TRC), Mhandisi,Ayubu Mdachi, akizungumza na wafanyakazi  la shirika  la reli nchini namna  mradi huo unavyoendelea katika Lot 1 inayotoka Dar es Salaam mpaka Morogoro.
wafanyakazi  la shirika  la reli nchini wakiangalia reli ya kisasa ya SGR kwenye eneo la Soga mkoa wa Pwani.
Picha ya pamoja
Ujenzi wa  mradi wa reli SGR  ukiendelea katika eneo la Stesheni jijini Dar es Salaam.Muonekano wa sehemu ya nguzo za mradi wa Standard Gauge.  Sehemu ya reli ambayo imekamilika.Muonekano wa Stesheni ya Pugu ikiwa bado inaendela kujengwa. Mafundi Wakiendelea na Ujenzi wa Madaraja na kalavati katika eneo la mradi wa SGR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...