Mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, Upendo Sanze, akifafanua jambo kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibakwe, wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma, kuhusu umuhimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati. 
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibakwe, wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma, wakimsikiliza Mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, Upendo Sanze (hayupo pichani), alipofika shuleni hapo kuhamasisha umuhimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
 Mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, Salome Majala, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibakwe, wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma, ili kuwahamasisha kusoma masomo ya Sayansi na Hisabati. 
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibakwe, wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma, Bw. Sajigwa Nikupala akisisitiza jambo kwa wanafunzi wake  wakati Wahandisi wanawake kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, walipofika shuleni hapo kuhamasisha umuhimu wa usomaji wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
Picha na WUUM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...