Na Woinde Shizza Globu ya jamii 

Watoa huduma za msaada wa kisheria nchini wametakiwa kutotumia nafasi yao ya kutoa msaada wa kisheria kufanya mambo kinyume na taaluma yao na maadili yao ya kikazi.

Hayo yamebainishwa Leo na Katibu mkuu wa wizara ya katiba na sheria prof  Sifuni Mchome wakati akiongea katika kongamano la Watoa huduma za msaada wa kisheria uliofanyika jijini Arusha ambapo alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha Watoa huduma hao kufuata maadili ya Kazi yao.

Alisema kuwa kwakuwa Watoa huduma wa msaada wa kisheria wanafanya Kazi kwa kujitolea hivyo ni wajibu wao kuzingatia maadili ,yanayoendana na Katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayotambua na kulinda haki za binadamu pamoja na kulinda tamaduni njema za kitanzania.

"Napenda kusisitiza msitumie mlango wa usaidizi wa kisheria kutumika kama vibaraka " alisema mchome.

Kwa upande wake Waziri wa katiba na sheria Balozi dkt Augustine Mahiga aliwataka Watoa huduma hii ya kisheria kutumia kikamilifu makubaliano yaliowekwa na utekelezaji wake usibaki katika karatasi bali wayafanyie Kazi kikamilifu ili wananchi wanaohitaji msaada wa kisheria waweze kufaidika nayo.

Aliongeza kuwa itakuwa haina maana kama sheria ,kanuni miongoni na makubaliano yaliopo hayata mnufaisha Mwananchi mhitaji wa huduma hii pia libainisha kuwa wakati pia serikali inaendelea kuimarisha mifumo ni vyema pia wahakikishe wanawafikia wananchi walio wanyonge katika maeneo yao.

Mahiga alisema kuwa serikali iko mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wananchi wanyonge wanathaminiwa nakupewa hadhi sawa na wengine ,na kwakutilia mkazo serikali imepitisha sheria ya msaada wa kisheria na itaendelea kuimarisha nifumo ya upatikanaji haki nchini ili huduma hii itolewekatika utaratibu na mfumo mzuri utakao wezesha kuwafikia wananchi kwa wakati na kwa ubora unaostaili.

Aidha aliwataka wasaidizi hawa wa kisheria kuendelea kusimamia misingi imara ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania inayotambua na kulinda haki za binadamu pamoja na kulinda tamaduni njema za kitanzania ambazo ndiyo tunu yetu tunayojivunia katika kulinda utu na heshima ya mtanzania .
 Waziri wa katiba na sheria Balozi Dkt  Augustine Mahiga akizungumza na  waandishi wa habari Mara baada ya kufungua kongamano
Msaili wa Watoa  huduma za msaada wa kisheria nchi bi.Felistas Mushi akizungumza na Waandishi mara baada ya ufunguzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...