Mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi,mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na naibu meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Lyata 
Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda akiwa na Mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi alipokuwa kwenye mkutano na walimu wazalendo mkoani Iringa kujadili maswala ya uzalendo wa wananchi wa Tanzania kwa nchi yao
Baadhi ya walimu wazalendo walihudhulia mkutano huo uliongozwa na Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda







NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

WAZIRI mkuu mstaafu Mizengo Pinda amewataka walimu wazalendo wa mkoa wa Iringa kujifunza uzalendo kuwa na uzalendo wa nchi yao ili kuendeleza umoja na mshikamano na amani iliyopo inayosaidia kuleta maendeleo bila kuwa na chuki na visasi ambavyo mara nyingi vimekuwa vikivuruga amani.

Akizungumza na baadhi ya walimu wa shule za sekondari na shule ya msingi mkoani Iringa waziri mkuu mstaafu mizengo panda aliwataka walimu hao kujifunza nini maana ya kuwa mzalendo na ndio silaha pekee ya kuhakikisha tunakwepa kuanzisha vita kwenye nchi hii.

Kuthamini vitu vilivyopo katika nchi yako ni moja ya kuwa mtanzania mzalendo kwa kuwa utakuwa unalinda mali za nchi na kuhakikisha amani inakuwepo kwa kuna wananchi ambao ni wazalendo na nchi yao bila kujali itikadi ya vyama vilivyopo katika nchi hiyo” alisema Pinda

Pinda alisaema kuwa nchi nyingi ambazo hazijaingia kwenye vita ni nchi zile ambazo zimekuwa zikibadilishana uongozi bila kutumia mabavu,hivyo utaona nchi nyingi zinapigana kwa ajili ya kugombea madaraka lakini hali tofauti kwa nchi ya Tanzania.

“Angalieni nchi kama Somalia tu hapo jirani wanavyopigana kwa ajili ya kugombea kuongoza nchi huo sio uzalendo wa wananchi wa Somalia ndio maana leo hii nawaambieni kuwa lazima mjifunze nini maana ya uzalendo ili kulinda na kuthamini amani ya nchi yenu” alisema Pinda

Pinda aliongeza kwa kusema kuwa uzalendo kwa wananchi wa Tanzania umeanza kupungua kwa kuwa watu wengi hawajui nini maana ya kuwa mazalendo hivyo wanatakiwa kujifunza katika umri huo kuwa wazalendo na nchi yao.

Pinda aliwata walimu kuanza kuwa na uzalendo kuanzia pale ulipozaliwa au ulipokulia ndio utaanza kuijenda nchi hii kwa kuwa umeenza kuthamini toka ulipokuwa mdogo hadi ukubwani kwa kuwa watakuwa na lengo la kulinda amani ya nchi.

“Uzalendo pia huanzia pale unapohuzulia mikutano ya hadhara kwa lengo la kujifunza na kujua muelekeo wa mtaani kwako au kujua mwelekeo wa taifa kwa kuwa kwenye kila mkutano wa hadhara kuna mambo ya msingi utajifunza tu” alisema Pinda

Naye mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi aliwataka walimu kuwa makini na viongozi ambao wanawachagua kwa kuwa ndio chanzo cha kuharibu maendeleo ya nchi kutokana na kiongozi huyo kutokuwa na uzalendo wan chi yao.

“Wananchi wanasababisha umasikini wenyewe kutokana na kuchagua viongozi ambao hawana uwezo ndio hupelekea umaskini katika kwa wananchi waliomchagua kiongozi waliyekuwa na imani naye,hivyo kukosea kuchagua kiongozi bora ni kujitafutia matatizo wenyewe” alisema Ngerera

Hapi aliongeza kwa kuwaambia walimu hao kuwa sehemu ya kumfundisha wananchi uzalendo ni katika umri mdogo hasa wanafunzi kwa kuwa ndio kipindi ambacho wengi wameanza kuwa na uelewa wa maisha ni nini.

“Jamani lazima mjifunze mnapotaka kumlaumu kiongozi mlimchagua wenyewe ni lazima mjipie wenyewe kwanza mlikosea wapi na sasa mnatakiwa mfanye nini ili kuhakikisha mfanya kazi huku mkiwa mmetawaliwa na uzalendo wenu” alisema Hapi

Kwa upande wake Mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi alimuakikishia waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda kuwa walimu wazalendo wamekuwa wazalendo kweli kweli kwa kuijenga Iringa mpya na kufanya kazi pamoja na serikali pamoja na chama tawala.
“Walimu unaowaona humu ndani wote ni wanachama wa chama cha mapinduzi na wapo tayari kukitumikia chama tawala kwa kuwa kinaongoza vizuri serikali kwa miaka yote” alisema Ngowi

Ngowi alisema kuwa walimu wazalendo wamekuwa wakifanya kazi ya kuutangaza uzalendo kwa wanafunzi na wananchi wote ambao wanatuzunguka kwa lengo la kufanya kazi pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli

“Rais wetu amekuwa akifanya kazi kwa kutunganisha watanzania wote kuwa kitu kimoja hivyo hata sisi walimu wazalendo mkoa wa Iringa tunamuunga mkono kwa kila jambo jema ambalo anaifanyia nchi yetu” alisema Ngowi

Ngowi alimazia kwa kumuomba waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda kuwafikishia salamu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kuwa walimu wazalendo mkoa wa Iringa wapo makini na wapo tayari kufanya kazi pamoja naye kwa kila jambo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...