Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako leo ametembelea
na kukagua hatua za maandalizi ya ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la Chuo Kikuu
Mzumbe Kampasi ya Mbeya, ambapo amepongeza Uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa hatua
za ujenzi ulipofikia.
Akiwa ameambatana na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Lughano Kusiluka, Prof Ndalichako
amemwelekeza Mkandarasi wa Ujenzi kuhakikisha kufikia Juni 2019 ujenzi wa Jengo hilo kuwa
umekamilika kama ilivyopangwa.
Kukamilika kwa ujenzi kutawezesha jumla ya wanafunzi 900 kupata vyumba vya madarasa
mbali na kumbi za mikutano na ofisi za uendeshaji. Jengo hilo linatarajiwa kuwekwa jiwe la
Msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Magufuli Mei
1, 2019.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako (katikati) akikagua mahali litakapojengwa jiwe la msingi ambalo litawekwa
rasmi na Rais wa Jamhuri wa Muuungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Mei 1,
2019. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka na kulia ni
Mkadarasi wa Ujenzi Injinia Thedeus Koyanga (mwenye shati la mikono mirefu) akifuatiwa na Profesa
Ernest Kihanga Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha.

Waziri Ndalichako akiongozwa na Mkandarasi wa mradi akikagua vyuma vya madarasa mara
alipowasili kukagua ujenzi wa jengo la ghorofa tano la Taaluma na Utawala linalotazamiwa kumalizika
mwezi Juni,2019. Pamoja naye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka, Naibu
Mawakamu Mkuu wa Chuo Utawala na fedha Prof. Ernest Kihanga na wasimamizi wa ujenzi.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiweka saini kwenye
kitabu cha wageni kwenye eneo la ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la chuo Kikuu Mzumbe
Kampasi ya mbeya mara tu baada ya kuwasili. Aliyeshika kitabu ni Injiani Thadeus Koyanga na kushoto
anayeshuhudia tukio hilo ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka ( Mwenye
Kaunda suti kushoto).
Profesa Joyce Ndalichako alikagua muonekano wa nje wa jengo la Taaluma na Utawala la chuo
Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya pamoja na kukagua usafi wa mazingira, alipofanya ziara ya kukagua
maendeleo ya ujenzi kabla Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli hajafika kuweka jiwe la msingi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...