Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WAFANYABIASHARA na watumiaji wa soko la Buguruni jijini Dar es Salaam wameridhishwa na bei ya bidhaa sokoni humo hasa katika msimu huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza na Michuzi Tv Mwenyekiti wa soko la Buguruni,Said Habibu Kondo amesema kuwa bidhaa za kilimo zimeongezeka tofauti na kipindi cha nyuma hivyo wananchi wasiogope kupanda kwa bei za bidhaa katika msimu huu wa Ramadhani.

Amesema kuwa bidhaa zote zinanunulika kwa bei ya kawaida kabisa huku bidhaa nyingine zikishuka bei na zinapatikana kwa urahisi zaidi.

Kwa upande wao wafanyabiashara wa soko hilo wamesema kuwa shughuli katika soko hilo zinaendelea kama kawaida na hawajapata malalamiko ya kupanda kwa bei za bidhaa sokoni humo.

Mmoja wa wateja akizungumza na blogu ya jamii amesema kuwa bidhaa nyingi za kilimo zinapatikana zikiwemo viazi, maboga, mihogo na magimbi na bei zake ni za kawaida kabisa na kila mwananchi anaweza kuzimudu.
Mwenyekiti wa soko la Buguruni,Said Habibu Kondo akizngumza na Michuzi Tv leo jijini Dar es Salaam juu ya bidhaa zote zinanunulika kwa bei ya kawaida kabisa huku bidhaa nyingine zikishuka bei na zinapatikana kwa wingi.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

wafanyabiashara wa soko la Buguruni wakiendelea na kazi kama inavyo onekana katika picha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...