Kampuni
inayotoa huduma za usafiri kwa njia ya mtandaoni nchini - Bolt
imezindua kitufe cha dharura (SOS) kwa lengo la kuimarisha usalama wa
madereva kipindi wanapokutana na hatari yoyote.
Akizungunza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salamaam Meneja wa Bolt
Tanzania Remmy Eseka alisema madereva wanaotumia programu hiyo ya Bolt
sasa wanaweza kutumia huduma hiyo mpya ya usalama muda wowote watakapo
hisi kuwa wapo hatarini au eneo ambalo si salama.
Alisema
matumizi hayo ya kitufe cha dharura dharura (SOS) yamekuwa kama
muendelezo wa Bolt kutumia teknolojia kuimarisha usalama wa madereva
wanapokuwa barabarani.
"Usalama
wa dereva na abiria ni swala la muhimu sana kwetu. Tunaongeza safu ya
usalama wa dereva zaidi ya ule uliopo tayari wa kufutalia mubashara
safari kwa kutumia GPS na mfumo wa thathmini.
"Kitufe
cha dharura (SOS) kilichopo kwenye programu ya Bolt ya dereva,
huwezesha taarifa kuwafikia kampuni ya ulinzi ya SGA Tanzania Limited,
kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma hizi Afrika Mashariki" alisema
meneja kampuni hiyo ambayo zamani ilifahamika kwa jina la Taxify
Aidha,
Meneja wa mauzo na masoko kutoka SGA, Faustina Shoo akisem kitufe cha
dharura (SOS) kilichowekwa kwenye programu ya madereva kinapotumika,
simu hupelekwa kwenye kituo cha dharura cha SGA, ambao baada ya kuhakiki
uhalali wa dereva, wanapeleka gari la wagonjwa au timu ya askari
kuelekea alipo dereva kuweza kumsaidia kama watoa huduma wa kwanza.
"Bolt italipia gharama hizi pamoja na gharama zitakazo pitishwa kwa kila tukio.
Tunaendeleza
nia yetu ya kujibu mahitaji ya wateja/wabia kwa kutoa huduma ya uokoaji
wa dharura kwa madereva wa Bolt kutokana na ubia huu. "Madereva
wa Bolt wanahakikishiwa kupata huduma ya masaa 24 kupitia kitengo chetu
cha dharura iwapo watapata tatizo wakiwa safarini.” alisema.
Mmoja wa abiria wanaotumia programu ya Bolt, akipata huduma kutoka kwa dereva bodaboda baada ya Bolt
zamani Taxify inayotoa huduma za usafiri kwa njia ya mtandaoni nchini
kuzindua kitufe cha dharura (SOS) jijini Dar es salaam jana kwa lengo
la kuimarisha usalama wa madereva kipindi wanapokutana na hatari yoyote.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...