Anaandika Abdullatif Yunus, Michuzi TV - Kagera.

Hali ya Miundo mbinu na maeneo korofi ndani ya Manispaa ya Bukoba, imeanza kuimarika baada ya Mvua kubwa iliyonyesha Mei 26, 2019 na kusababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo mengi Mjini humo.

Mvua hiyo iliyoanza kunyesha majira ya Asubuhi saa mbili, na kisha kukatika baada ya muda wa lisaa moja, mpaka sasa inasubiriwa ripoti rasmi kufahamu ni athari kiasi gani na madhara yaliyotokana na mafuriko hayo, ingawa duru zinaeleza kuwepo kwa kifo cha mtoto mmoja, upotevu na uharibifu wa Mali nyingi kufuatia mafuriko hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brig. Gen Marco E. Gaguti amekaririwa katika ukurasa wake wa Twitter akiandika kuwa " Hali imeendelea kumarika baada ya Mafuriko ya Jana Tarehe 26 MRI 2019. Tuendelee kuchukua tahadhari kwani Mvua bado zipo. Aidha tuzingatie kanuni muhimu za Afya kuepuka magonjwa ya Mlipuko".

Katika ujumbe huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Uslama Mkoa Mhe. Gaguti Ameweka baadhi ya Picha zikionesha maeneo yaliyokuwa korofi na kushindwa kupitika Jana kufuatia wingi wa Maji na sasa yanapitika vizuri na shughuli nyingine za kijamii zinaendelea kama kawaida.
 Muonekano wa hali ilivyokuwa Jana na Leo, katika Daraja eneo la Lina's Hotel  baada ya hali kuimarika.
 Daraja la Kanoni maarufu kwa wauza senene muonekano wa Jana na Leo.
 Pichani Rc Gaguti akionekana kukatiza  viunga mbalimbali Manispaa ya Bukoba kujionea hali ilivyo kufuatia Mvua kubwa iliyonyesha Tarehe 26, Mei 2019 na kusababisha Mafuriko.
Moja kati ya madaraja mengi ya watembea kwa miguu, linalopatikana maeneo ya Rwamishenye Machinjioni, kuelekea Kyebitembe hali iko hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...