KANLESA wa nchini Ujerumani Angela Merkel
ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima ya
Chuo Kikuu maarufu cha Harvard.
Rais wa Chuo cha Havard Larry Bacow ambaye
ndiye aliyemtunukia Merkel tuzo hiyo amesema
kuwa Kansela huyo wa Ujerumani ni mwanasiasa
mwenye nguvu barani Ulaya.
Wakati wa sherehe za kutunukiwa kwa Shahada
hiyo ya Udaktari, chuo hicho kimemsifu Merkel kwa
matamshi yake "Tutaweza kulisimamia hili" wakati
wa mgogoro wa wakimbizi ulioanza mwaka 2015
nchini Ujerumani wakati aliporuhusu idadi kubwa ya
wakimbizi na kukabiliwa na ukosoaji mkubwa nchini
mwake.
Akizungumza kwenye hotuba yake kwa wanafunzi,
wakati wa mahafali ya 368 ya chuo hicho cha
Havard, Merkel amewaonya wanafunzi dhidi ya
kuchanganyikiwa na kuuchukulia uongo kuwa ukweli
na ukweli kuwa ni uongo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...