Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Zoezi la kuhesabu kura za uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Yanga umemalizika na Dr Mshindo Msolla kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga kwa jumla ya kura 1276 katika Uchaguzi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Msolla amembwaga mpinzani wake Dkt Jonas Tiboroha aliyepata kura 60 huku kura 5 zikiwa zimeharibika.Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Fredirick Mwakalebela amefanikiwa kushinda nafasi hiyo baada ya kupata jumla ya kura 1206 kati ya kura 1341.

Mwakalebela amewapiku wenzake wanne ambao wote walikuwa wanawania nafasi hiyo kwa kura nyingi.Wagombea hao Titus Osoro alipata kura 17, Yono Kevela kura 31, Chota kura 12 na Janeth Mbeni akipata kura 61 na kura 21 zikiwa zimeharibika.

 Katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji waliochaguliwa ni Hamad Islam 1206, Engineer Mwaseba 1174, Dominick Ikute 1088, Kamugisha Kalokola 1072, Arafat Haji 1024, Salum Ruvila 976,Saad Khimji 788 na Rodgers Gumbo 776

Uchaguzi Mkuu wa Yanga umefanyika leo kwenye ukumbi wa Police Officers Mess Oysterbay na jumla ya wanachama 1341 walijitokeza kupiga kura.
Dr Mshindo Msolla Mwenyekiti mteule wa Klabu ya Yanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...