Na Humphrey Shao, Globu ya Jamiii
Wito
umetolewa kwa Serikali na watunga sera kuhakikisha wanapitia upya na
kufanya mabadiliko katika sheria ya usalama barabarani hili kuweza
kudhibiti ajali zinazotokana na uzembe wa watu kwa makusudi.
Wito
huo umetolewa jijini Dar es Salaam leo na Kaimu Mkurugenzi wa Chama cha
Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA),Mary Richard alipokuwa akizungumza
na Waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani
kwa umoja wa mataifa.
"sheria
hiyo kwa sasa ina mapungufu mengi kiasi mtu akikutwa na kosa adhabu
zake ni za kawaida na makosa mengi yamebainishwa katika kanuni badal aya
sheria yenyewe ametaja sheria hii inamtaja mtu aliyekaa siti ya mbele
na Dereva ndio wanapaswa kufunga mkanda wakati kanuni inataja abiria
wote wafunge mkanda jambo ambalo lina ukakasi kidogo"amesema Mary.
Mary
ametaja kuwa sheria hii ya Sasa inaseama Dereva wa pikipiki ndio
anapswa kuvaa kofia ngumu peke yake wakati sasa jeshi la Polisi ketengo
usalama barabarani wameweka kanuni Dereva na abairia ndio wanapaswa
kuvaa kofia hivyo ni bora vitu vyote hivi vingewekwa kwenye sheria hivyo
tunaomba mamlaka zinazousika pamoja na Wizara ya Mambo ya ndani
waangalie utaratibu wa kubadilisha sheria hii.
kwa
upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma , Fatma Toufiq amesema
kuwa ajali za barabarani zinaepikika kama watanzania wote wataweza
kufata sheria na kuwa makini pindi wanapoendesha vyombo vya moto.
amesema
kuwa yeye kama mbunge anayeshiriki katika kutunga sheria atasimama
kidete kuhakikisha sheria hii mpya ya usalama barabarani inapatikana hli
tuweze kupunguza takwimu za ajali na walemavu wakudumu wanaotokana na
ajali za barabarani
Kaimu
Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA),Mary
Richard akizungumza na Waandishi juu wiki ya usalama barabarani
Mbunge
wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma , Fatma Toufiq, akieleza ushuhuda wake
kwa waandishi wa habari juu ya ajali ilivyoweza kumletea cahangamoto ya
utendaji katika kazi
Mratibu
wa Usalama Barabarani kutoka shirika la umoja wa Mataifa la WHO,Mary
Kessy akizungumza mpango wa shirika lake katika kudhibiti usalama
barabarani
Muwakilishi
wa Mabalozi wa Usalama Barabarani(RSA),John Seka akieleza namna taasisi
yao ilivyojipanga na inavyoshirikiana na jeshi la Polisi kutoa taharifa
za watu wanaokiuka sheria za Usalama Barabarani
Sehemu
ya Waandishi wa habari walioshiriki Mkutano kuhusu Masuala ya Usalama
barabarani leo jijini Dar es Salaam uliofanyika katika ukumbi wa Tamwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...