TIMU Four Ways Park Fc yenye makazi yake Kinondoni jijini Dar es Salaam na Girls Queens yenye makazi yake Msimbazi Kariakoo jijini Dar es Salaam wameingia kambini leo rasmi kujiandaa na mashindano ya Castle Africa 5s(5 – aside) yanayotarajia kuanza kutimua vumvi Juni 7 na 8,2019 katika Uwanja wa Taifa wa Zamani(Shamba la Bibi) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Balozi wa Castle Lager Africa nchini Tanzania, Ivo Mapunda amesema timu zote ziko vizuri tayari kwa kuwakilisha Watanzania katika fainali za Kimataifa na ushindi ni lazima kulingana na maandalizi waliyonayo na watakayoendelea nayo.

Mwaka huu Tanzania tutawakilishwa na timu ya Wanaume kutoka Four Ways ya Kinondoni na timu ya Wanawake ya Girls Queens kutoka Msimbazi Kariakoo kwa ujumla timu zote ziko sawa na ziko tayari kwa fainali hizo na leo rasmi sasa wanaingia kambini kwa kujiandaa na fainali hizo.

Nae Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli alizitaji Nchi shiriki zinazotarajiwa kushiriki mashindano hayo ya Africa 5s kuwa ni Africa Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Lethoto, Uganda, wenyeji Tanzania na chi alikwa ya Nigeria.

Kikuli alisema Nchi hizo zikiwakilishwa na timu ya Wanaume na Wanawake zinatarajiwa kuwasili nchini Juni 5,2019 tayari kwa fainali za Castle Africa 5s.Juni 6,2019 timu zitakabidhiwa vifaa vya michezo katika Hoteli ya Lamada jijini Dar es Saalaam tayari kwa kuanza mashindano rasmi Juni 7 na 8,2019.

Tunawaomba watanzania wapenda michezo wajitokeze kuja kuzishangilia timu zao zinazowakilisha nchi katika Fainali hizo za Castle Africa 5s.Mwisho Kikuli alisema fainali hizo zinatarajiwa kuhudhuria na Balozi wa Castle Africa 5s, Samwel Eto’o hivyo tujitokeze kwa wingi kuja kumshuhudia mchezaji mkongwe wa Zamani pamoja na kupiga nae picha.

wameibuka mabingwa katika Bonanza kubwa la Soka lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Posta Kijitonyama kwa udhamini wa Kampuni ya Bia nchini (TBL) kupitia bia yake ya Castle Lager na hivyo kuzawadiwa Kikombe, Medali za dhahabu, Pesa taslimu shilingi 1,500,000/=, Caton ya bia ya Castle Lager pamoja na kuwakilisha nchi katika fainali za Caslte Africa 5s zinazotarajiwa kufanyika mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo.
Baloziwa Castle Lager Africa 5s, Ivo Mapunda (kushoto) akizungumza na wachezaji wa timu ya Four Ways Fc ya Kinondonina Girls Queens ya Msimbazi Kariakoo zinazowakilisha nchi kwenye fainali za mashindano ya Castle Africa 5s wakati wa uzinduzi wa Kambimaalumu ya maandalizi ya mashindano hayo yanayotaraji wakufanyika Juni 7 na 8,2019 katika Uwanja Taifawa Zamani jijini Dar esSalaam. Jumlaya Nchinane(8) zinatarajiwa kushiriki fainali hizo mwenyeji akiwani Tanzania.
Wachezaji wa Four Ways Fc ya Kinondonina Girls Queens ya Msimbazi Kariakoo zote za jijini Dar es Salaam wakifanya mazoezi wakijiandaa na fainali za mashindanoya Castle Africa 5s yanayotarajiwa kufanyika Juni 7 na 8,2019 katikaUwanjaTaifa wa zamani nijijini Dar esSalaam. Jumla ya Nchi nane(8) zinatarajiwa kushiriki fainali hizo mwenyejiakiwani Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...