Na Agness Francis, Michuzi Tv
Mwenyekiti wa bodi ya magavanazi wa taasisi ya ustawi wa Jamii Sophia Simba leo amefungua kongamano la mkutano wa kimataifa inayoshuhulika na maswala ya ustawi wa jamii ili kuleta chachu ya maendeleo endelevu ya uchumi wa viwanda, ambao umehudhuriwa na watu kutoka Sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi utakao malizika mei 10 mwaka huu.
Sophia Simba amezungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo ambapo amesema kuwa mkutano huo una lengo la kujua ni jinsi gani maswala ya ustawi wa jamii utakavyo saidia katika kukuza uchumi na mabadiliko ya viwanda hapa nchini.
Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa ni vizuri jamii ikaelewa hata nchi nyingine duniani kama Korea, China na Malaysia wamepitia misukosuko mingi mpaka hapo walipofikia kwa kujitolea kwa hali ya juu.
"Juhudi ambazo zinafanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ni kuhakisha tunafika pale tunapokakusudia kama tukiwa wote tunapeleka elimu Katika jamii, na serikali imekuwa ikitekeleza mpango wa sheria na taratibu mbali mbali zilizopo ili kulinda ustawi wa jamii katika utendaji wake wa kazi"amesema Sophia Simba.
Vile vile ameongezea kwa kusema kuwa Taasisi ya Elimu ya juu ikiwemo na ya ustawi wa jamii zinawajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba taaluma hiyo inatoa mchango mkubwa katika kuleta mapinduzi ya viwanda hapa nchini.
Hata hivyo Makamu mkuu wa Taasisi ya mipango, fedha na utawala Zena Mabeyo amesema kuwa inatakiwa tuwe na rasilimali watu kuweza kuwashawishi watu kuwa na mfumo bora ili kuweza kuwafikia wananchi katika safari ya kuelekea kuboresha Tanzania ya viwanda.
"Hatuishii hapa tu kwa kadri ya miaka inavyozidi kuendelea tutakuwa tunaandaa makongamano ya aina hii yatakayoangalia michango ya fani nyinginezo katika kutoa mchango wa nchi.
Pia Mabeyo amemalizia kwa kusisitizia usalama na ulinzi kwa wazee, watoto pamoja na watu wenye ulemavu katika kuleta mapinduzi ya uchumi wa Viwanda tukiamia kila mtu ana mchango katika kuleta maendeleo.
Mwenyekiti wa bodi ya magavanazi wa taasisi ya ustawi wa Jamii Sophia Simba akizungumza wakati wa uzinduzi na wadau mbali mbali leo Jijini Dar es Salaam waliohudhuria Kongamano hilo linaloshughulika na maswala ya ustawi wa jamii ili kuleta chachu ya maendeleo endelevu ya kukuza uchumi wa viwanda hapa nchini.
Mwenyekiti mstaafu wa bodi ya magavanazi wa taasisi ya ustawi wa Jamii Lucian Msambichaka akizungumza na wadau mbali mbali katika Kongamano hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Makamu mkuu wa Taasisi ya mipango, fedha na utawala Zena Mabeyo akifafanua jinsi Taasisi ya Ustawi wa Jamii jinsi inavyoweza kufanya kazi zake kwa jamii leo Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kongamano hilo ambalo hufikia tamati Mei 10 mwaka huu.
Wadau kutoka sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi waliohudhuria leo Jijini Dar es Salaam Kongamano hilo linalolenga kuunga mkono juhudi za Rais wa amu ya tano John Pombe Magufuli za kukuza Tanzania ya viwanda.
picha ya Pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...