Na Ripota,Kimataifa 

VYOMBO vya habari vya nchini Korea Kusini vimeripoti kuwa Korea Kaskazini inadaiwa kumuua mjumbe wake maalumu kwa ajili ya Marekani Kim Hyok Chol baada ya kushindwa kwa mkutano wa pili wa kilele kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na rais Donald Trump. 

Kwa mujibu wa Gazeti la Chosun Ilbo limeandika Chol aliyeuandaa mkutano huo wa Hanoi na kumsindikiza Kim kwenye treni yake binafsi ameuawa kwa kupigwa risasi kwa kile kinachotajwa kumsaliti kiongozi huyo wa juu baada ya kufanikiwa kuishawishi Marekani wakati wa majadiliano ya kabla ya mkutano huo wa kilele. 

Gazeti hilo lililonukuu chanzo ambacho hakikutambulishwa limesema Chol, aliuawa Machi, katika uwanja wa ndege wa Mirim pamoja na maafisa wanne waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje baada ya uchunguzi. 

Mkalimani wa Kim kwenye Umoja wa Mataifa naye ametiwa kizuizini baada ya kufanya makosa kwenye mkutano huo wa kilele. 

CHANZO-DW

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...