Na Ripota,Kimataifa 

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi(UNHCR) limewasafirisha kwa ndege wakimbizi na wahamiaji wapato 150 kutoka Mji Mkuu wa Libya Tripoli, kuelekea katika Mji 

Mkuu wa Rome nchini Italia. 

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji (BBC) ni kwamba waliochukuliwa ni raia kutoka mataifa ya Eritrea, Ethiopia, Sudan na na wengi wanahitaji matibabu na wanakabiliwa na utapiamlo. 

Pia imeelezwa kuwa kuna raia wa nchi hizo ambao ndoto zao ni kwenda nchi za Ulaya lakini huishia nchini Libya ambako hushikiliwa kwenye vituo vya mahabusu katika hali mbaya.Inaelezwa kuwa takribani watu 600 wamepoteza maisha yao katika makabiliano ya hivi karibuni nchini Libya kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...