Na Woinde Shizza Michuzi TV, Arusha

Imebainika kuwa ili vita dhidi ya ufisadi, rushwa pamoja na wizi wa rasilimali za taifa ziweze kuisha ni lazima kushirikisha makomandoo saba ambao niwazoefu. 

Hayo yamebainishwa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania (KKKT)dayosisi ya Karagwe Dkt. Benson Bagonza wakati akizungumza katika kongamano la vijana lililoandaliwa na Taasisi ya Change Tanzania lililofanyika jijini hapa. 

Aidha alitaja makomandoo hao saba kuwa ni mitandao ya kijamii, vyombo Huru vya Habari, Asasi za Kiraia, Taasisi zisizokuwa za Kiserikali, Vyama vya Vafanyakazi, Vyama vya Upinzani, Bunge Huru pamoja na Katiba Huru. 

Alisema kuwa matumizi chanya ya mitandao ya kijamii ni nyenzo nzuri ya utetezi katika jamii ila wasioliona hili ni Wale wanaothani kuwa nafasi zao ni msaada tosha na hawaitaji watetezi. 

"Taifa la Tanzania chini ya serikali ya awamu ya tano imetangaza Vita dhidi ya mafisadi, rushwa pamoja na wizi wa rasilimali za taifa na ili kushinda vita hii Serikali yetu inaitaji Msaada wa makomandoo wazoefu katika Vita hii "Alisema Bagonza

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Change Tanzania Forum  Maria Sarungi Alisema kuwa licha ya kuwa na sheria  juu ya uhuru wa kujieleza katika Mitandao lakini bado mitandao ya kijamii haikwepeki. 

Alibainisha kuwa wao kama Change Tanzania wanaendelea kusaidia uwepo wa uhuru wa kujieleza lakini wanataka badala ya kuchukuliwa hatua watumiaji hawa wa mitandao wapewe elimu Kwanza.
Askofu wa Kanisa la kiinjili na kilutheri Tanzania Dayosisi ya Karagwe Dkt. Benson Bagonza akiongea katika kongamano la vijana
Rais wa zamani wa Chama cha Wanasheria Fatma Karume akizungumza katika kongamano hilo ambapo aliwataka waandishi wa habari kutoogopa na kuwaeleza ukweli viongozi wao, pamoja na kufukua uwovu wote unaofanywa na viongozi wao. 
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Change Tanzania Forum  Maria Sarungi akizungumza na waandishi wa habari walivojipanga katika utoaji wa elimu katika masuala mbalimbali.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...