Na Editha karlo wa blog ya jamii,Kigoma
MKUU wa Wilaya ya Kigoma Samson Hanga ametangaza msako mkali wa kuwasaka wanaume wanaojipaka oil mwilini kisha kuwaingilia kingono kinguvu akina mama sambamba na kuwajeruhi na kuwaibia mali zao maarufu 'tereza' waliopo Mkoani Kigoma.
Anga aliyasema hayo juzi kwenye viwanja vya mwanga center wakati kanisa la halisi la Mungu baba likiwa kwenye kongamano lake lake la hija ambapo Mkuu huyo wa Wilaya alimuwakilisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia mstaafu Emanuel Maganga kwenye hija hiyo.
Hanga aliliomba kanisa hilo kufanya maombi maalum kwaajili ya pepo hilo teleza linalowasumbua wanawake liteketezwe."Hili suala la tereza hapa Kigoma lipo muda mrefu toka mwaka 2016 ila watu walikuwa wakilizungumzia kama vile siyo tatizo kubwa nina waomba katika maombi yenu mliombee na hili la tereza ili liishe hapa kwetu"alisema
Akiongoza maombi hayo ya kumteketeza teleza baba mtakatifu wa kanisa la Mungu baba Elisha Elia alisema tatizo la teleza katika Mkoa Kigoma limekwisha hivyo kila mmoja napaswa kuomba ili tatizo hili lisiendelee.
"Hawa mapepo wachafu teleza wanaojipaka oil ili wakishikwa wateleze tunakuomba Mungu baba ukaondoe roho hii ya pepo mchafu huyo teleza atoweke na asirudi tena kuwatesa watu wako hasa wanawake wa Kigoma"aliomba baba mtakatifu
Katika kuhakikisha maombi yao yanamfikia Mungu baba aliwataka waumini wote waliokusanyika katika viwanja vya mwanga center kulala chini kifudifudi nakumuomba. Mungu kwa dakika tatu ateketeze pepo la teleza kwenye Mkoa wa Kigoma.
Mkuu wa polisi wa Wilaya ya ya Kigoma Raphael Mayunga amesema kuwa jeshi la polisi mpaka sasa tayari linawashikilia watu kadhaa kwa tuhuma hizo na kuwataka wananchi kufika kituoni waweze kuwatambua.
"Wale waliofanyiwa vitendo hivyo wanaweza kufika hapa ili waweze kuwatambua,kama mtu anaogopa anaweza kuja kunifuata kwa siri aje kuwatambua"alisema.Alisema askari polisi wanafanya misako katika mitaa mbalimbali ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Teleza ni jina linalotumika kuwatambulisha vijana wanaofanya vitendi vya uhalifu nyakati za usiku ambao huvunja milango na kuwabaka wanawake kinguvu,kuiba na kuwajeruhi.
Baadhi ya waumini wa kanisa la halisi la Mungu baba wakiwa wamelala chini kwaajili ya maombi maalum ya kukemea pepo la kubaka wanawake,na kujeruhi"teleza"wakati wa ibada ya hija iliyofanyika katika viwanja vya mwanga center Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...